Royal Tour ingekuwa na tija kama Rais Samia angeambatana na Mumewe, watoto wake angalau wawili na kushirikisha wasanii maarufu wa Kitanzania

Royal Tour ingekuwa na tija kama Rais Samia angeambatana na Mumewe, watoto wake angalau wawili na kushirikisha wasanii maarufu wa Kitanzania

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
4,035
Reaction score
11,462
Mambo mengine yanafurahisha sana. Huenda bado tupo nyuma ya muda ama hatujui tunatafuta nini.

Rais ametuambia kuwa yupo katika majukumu ya kurekodi kipindi maalumu ya royal tour chenye lengo la kutangaza vivutio vya utalii wetu kimataifa.

Mimi sijaelewa lengo na dhumuni maana siamini kama Rais ana umaarufu wa kuweza kuwapa tensioni hata watu milioni 40 nje ya Tanzania. Wanangu niwambieni ukweli nchi hii haina Mtu mwingine maarufu zaidi ya Diamond a na Mbwana Samatta.

Pili Rais kama Rais nje ya ofisi umaarufu wake utaletwa na maisha yake na familia hiyo kukosena kwa watu hao ni mambo ya aibu sana.

Bora hata wangemuweka mwanetu SNOOPY DOGY mambo yangekuwa supa.
 
Mama kawa msanii Ili apate Hela za kuwalipa polisi na wanajeshi, wahisani endeleeni kubana hivyo hivyo.
 
Hv unadhan Huyo Diamond na Samata wanaushawish mkubwa ulaya , hoja yako ingekua na nguvu May be ungesema wangemueka celebrity Kama Beyonce au Jay z hat wakina Serena Williams
Point muhimu. Kweli mtu mmoja maarufu kwa tangazo moja tu anaweza kuwa na impact kubwa sana.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Ujinga haujawahi kuisha hii nchi
 
Sijui kwenye kipengele cha Demokrasia Rais atachukua vile vyama vya vikaragosi wa CCM na wanachadema wa CCM? Atawezaje kuvijumuisha vyama vya siasa kabla ya kukutana navyo?
 
Ndani ya siku mbili tu baada ya kuapishwa tayari dunia ikaanza kumwongelea rais Samia. Akina Diamond wanajulikana Afrika, Samatta anajulikana kwenye ligi anayochezea lakini umaarufu wa rais SSH hauna mipaka.
Halafu ni issue sensitive sana kumwona rais anafanya matangazo kama hayo. Wengi watavutiwa na wanasubiria kwa ham kuona atawaonyesha nini.
 
Ata Rwanda waliamza wenyewe na tallest guy. Kwa watz wanavyo piga kelele za kukosoa uongozi ivi ww ungesikia serikalnimemlipa Messi atangaze utalii wa Tz ..lzm ww ungekuwa miongon mwa wa Tz wangepinga

Kuhusu wasanii wa ndani, ivi haukumbuki Kigwa alitumia wasanii wa bongo movie kutangaza ile #Taznania unforgetable lkn in return nini kikitokea ?
 
Mambo mengine yanafurahisha sana. Huenda bado tupo nyuma ya muda ama hatujui tunatafuta nini.

Rais ametuambia kuwa yupo katika majukumu ya kurekodi kipindi maalumu ya royal tour chenye lengo la kutangaza vivutio vya utalii wetu kimataifa.

Mimi sijaelewa lengo na dhumuni maana siamini kama Rais ana umaarufu wa kuweza kuwapa tensioni hata watu milioni 40 nje ya Tanzania. Wanangu niwambieni ukweli nchi hii haina Mtu mwingine maarufu zaidi ya Diamond a na Mbwana Samatta

Pili Rais kama Rais nje ya ofisi umaarufu wake utaletwa na maisha yake na familia hiyo kukosena kwa watu hao ni mambo ya aibu sana.

Bora hata wangemuweka mwanetu SNOOPY DOGY mambo yangekuwa supa.
Samatta ndiyo nani?
 
Back
Top Bottom