Royal Tour itampaisha Rais Samia na kuipaisha Tanzania kimataifa

Royal Tour itampaisha Rais Samia na kuipaisha Tanzania kimataifa

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
18,487
Reaction score
13,611
Wakosoaji wanasema zimetumika zaidi ya shilingi bilioni tano katika kuiandaa Royal Tour huko mbugani.

Yameongewa mengi, mengine ni mbwembwe tu kama ile habari ya Samia kuendesha gari kwa mara ya kwanza baada ya miaka 15 siku alipomuendesha yule mzee wa kizungu kule mbugani.

Mengine ni habari makini kwa maana ya kuitambulisha Tanzania kwa ukaribu zaidi kwa mabilioni ya raia wema wa dunia hii. Hakuna kitu muhimu katika dunia ya utalii na dunia ya kiuchumi kama kuijenga upya taswira nzima (image restructuring). Ni kitu cha kwanza kabisa katika soko zima la utalii.

Kwamba kila mtu huko Ulaya na kwingineko anajua kuwa Mlima KIlimanjaro upo Kenya leo hii Rais wa Nchi kwa kupitia kipindi maalum anachukua muda wake katika kuikanusha habari hiyo kwa vitendo. Zile habari za uongo zilikuwa zikitumiwa na majirani zetu kana kwamba sisi hatujui faida ya utalii katika uchumi mpana ni zipi!.

Hivyo Royal Tour inakwenda kurekebisha mtazamo mzima wa utalii na ule mtazamo wa aina ya watu wanaoishi katika hiyo Tanzania.

Naiona hii Tour ikienda kumpaisha zaidi Rais Samia kwa maana ya upande mzuri wa kwake (positive image). Unaweza kujulikana kwa kuua watu kama alivyokuwa maarufu Hitler. Unaweza kujulikana kwa unyama wa kutesa raia wa nchi yako mwenyewe wanaokupigia kura, huo pia ni umaarufu ingawa unachafua taswira nzima ya kiongozi na nchi anayoiongoza.

Ninaifananisha Royal Tour na ile biashara kati ya serikali ya Rwanda na timu za Arsenal na PSG. Kwamba mwanzoni hatukuwa tumemuelewa Paul Kagame ana lengo gani la kuingia mkataba mkubwa na vilabu vikubwa vya Ulaya. Lakini baada ya kuona maneno Visit Rwanda mgongoni mwa jezi ya Messi na Neymar ndio tukafahamu ni kwa namna ipi nzuri dunia inakwenda kuifahamu Rwanda na Kagame mwenyewe.

Hizi pesa shilingi bilioni tano sio chochote kulinganisha na ushawishi chanya tunaokwenda kuupata huko duniani. Sio chochote sio lolote kulinganisha na wingi wa watalii wanaokuja ambao baadhi yao ni wawekezaji wanaofanya biashara na mataifa mbalimbali duniani. Humo humo katika wanaovutiwa na Royal Tour kwa sasa wamo wawekezaji wenye viwanda halisi wanaofikiria kuja Tanzania.

Rais Samia na awe amejifunza sababu za kuwa mkali kwa walio chini yake watakaofanya madudu kama sehemu ya maisha yao. Wapo wenzetu wanaoshindwa kwenda na kasi ya huu ushawishi wa kidunia tunaoupata kwa sasa ni wale wale business as usual. Wakwamishaji wa shughuli za kimaendeleo wa kudumu!.

Rais na awe mkali, vinginevyo maana nzima ya muda aliotumia katika kuandaa hii Royal Tour unaweza kupotea bure. Pia atumie nafasi yake kwa ajili ya kuandaa mtazamo wa pamoja wenye kuelezea ni nini Royal Tour, nani wanategemea kufaidika nayo.

Maana Tundu Lissu ameshaanza upotoshaji ambao ukidakwa na wasomi wetu wa Twitter na Facebook tunaweza kupoteza mjadala wa lengo la Tour yenyewe, ni rahisi kuzama katika suala la wafaidikaji wa hii Tour wa leo hii tukisahau kuwa mfaidikaji mkubwa ni Tanzania kuchukuliwa kwa mtazamo chanya huko ughaibuni.

Kwamba pesa kwa leo hii zipo na thamani yake ipo, lakini heshima ya kiongozi wetu ya kudumu ni njema kuliko ingizo la mabilioni ya benki. Heshima yetu kama taifa na ulimwengu kuujua ukweli kuhusu mbuga zetu na mlima Kilimanjaro ni masuala yenye thamani kuliko ingizo la pesa.

Wanasiasa wamejaa upotoshaji wa kisiasa, wanajua wakipata public support malengo yao yatatimia, wataendelea kutanua mijini. Tuitazame Tanzania ya miaka kumi na tano ijayo kwa umakini mkubwa.
 
Njaa inasumbua sana, naona mtu anaitwa primitive alafu anatabasam, baadaye akiwa pembeni anaraumu ooh nimedhalilishwa, kisa ni mkate, unaandika mada ili usifie alafu iweje yaani!.
 
Ipo haja ya uanachama wa JF upimwe kwa kigezo cha elimu. Tuwe tunaweka vyeti vya shule. Sio mijitu mijinga na mipumbavu inakuwa member na kujaza uchafu humu. We mtoa mada ni mpumbavu kabisa.
Ulivyoandika tu unaonyesha kuwa wewe ni mmoja wa waliorudishwa mtaani baada ya kujipima na kujikuta hauna hadhi ya kukaa ofisini.

Royal Tour italipa tu, ni suala la uvumilivu wa sera na mipango ya kiserikali, kupingapinga unajitafutia maumivu ya moyo na mwisho ni kupata matatizo ya presha zisizokuwa na ulazima.
 
Back
Top Bottom