johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Tukio liko mubashara ITV
Rais Samia akiwa na mbunge wa Kawe wanahutubia wananchi wa jimbo la Kawe eneo la Tegeta manispaa ya Kinondoni.
Kwa sasa askofu Gwajima amepanda kwenye gari ya Ikulu na anatoa salamu za shukrani kwa Rais Samia kwa niaba ya wananchi.
Gwajima anasema wananchi wa Kawe siyo tu Wanampenda mama Samia bali wana mahaba naye.
Helicopter za polisi zinavinjari juu ya anga kuulinda mkutano huu mtakatifu.
Rais Samia amewataka wananchi waendelee kulipa kodi kwani kodi ni kwa maendeleo ya taifa.
Rais Samia amesema anaelekea Bagamoyo katika mtiririko wa uchukuaji picha ya filamu ya vivutio vya utalii wa Tanzania itakayozinduliwa nchini Marekani na kuonyeshwa dunia nzima.
Karibu
========
Katika ziara hiyo Rais Samia pia amekutana na Mbunge wa Kawe Askofu Gwajima, ambapo Rais ameuhoji umma: “Tunachanja, hatuchanji?” Huku wananchi wakitoa majibu tofauti.
Askofu Gwajima pia ameshukuru kwa kupata Bilioni 8 kwa ajili ya kurekebisha mitaro ya Kata ya Mbweni ili kudhibiti mafuriko kipindi cha mvua.
“Jambo lingine, ulitupa kila jimbo milioni 500 kwa ajili ya barabara lakini kwenye Jimbo la Kawe ukatupa bilioni 14, ambazo tunatengeneza barabara 115 za jimbo la Kawe za naani kwa mkono wa TARURA.”,
“Shida ya maji iliyokuwepo Nakasangwe, iliyokuwepo Kisanga, tayari matenki yameshajengwa katika maeneo mbalimbali na sasa kuanzia mwezi wa 10 tarehe 15 mradi wa maji yanayotokea Ruvu Chini utakuwa umeshafika Kawe.”