Tukio liko mubashara ITV
Rais Samia akiwa na mbunge wa Kawe wanahutubia wananchi wa jimbo la Kawe eneo la Tegeta manispaa ya Kinondoni.
Kwa sasa askofu Gwajima amepanda kwenye gari ya Ikulu na anatoa salamu za shukrani kwa Rais Samia kwa niaba ya wananchi.
Gwajima anasema wananchi wa Kawe siyo tu Wanampenda mama Samia bali wana mahaba naye.
Helicopter za polisi zinavinjari juu ya anga kuulinda mkutano huu mtakatifu.
Rais Samia amewataka wananchi waendelee kulipa kodi kwani kodi ni kwa maendeleo ya taifa.
Rais Samia amesema anaelekea Bagamoyo katika mtiririko wa uchukuaji picha ya filamu ya vivutio vya utalii wa Tanzania itakayozinduliwa nchini Marekani na kuonyeshwa dunia nzima.
Karibu