Royal Tour yahamia Chato

....suala la Tundu Lissu kupigwa risasi,Tundu Lissu anamficha dereva hadi leo na kaambiwa mlete dereva tutakutajia aliyekupiga risasi mahakamani lakini Lissu hataki
Kwa hiyo dereva anajua wale wauaji kuliko zile camera za cctv mlizoondoa na kuficha?!!!
Acheni unafiki..
Hizo stori za Ben Saanane kuonekana ni uongo mtupu.

Na wale wengi wa kwenye viroba je?

Na Azory Gwanda je?
 

Dereva ndio afanyeje?. Yani siku hizi mhanga ndio mwenye kufanya upelelezi?. Sheria gani inasema hivyo. Uzuri mhusika mkuu naye aliondoka kwa aibu, damu ya mtu ni nzito. Nyie endeleeni na porojo.
 
Ni kweli hata mi nilienda kimya kimya. Ukitaka kufika kuhiji pitia ofisi ya mkuu wa wilaya upate security clearance (maana wale vichaa wa humu JF hawapaswi kabisa kufika huko). Hakika kaburi lake limejengewa vizuri sana na ndani kuna makaburi ya baba yake na dada yake nadhani na mtoto wake. Pia kukamilika kwa nyumba yake ya kumbu kumbu ni vizuri mno.
 
Semeni mna hasira watu wapo busy na Simba na Yanga hizi siku mbili na kusahau Kama ni miaka miwili ya Magufuli kufa.
 
Kristo alitukanwa, alikashifiwa, alidhalilishwa (fikiria mpaka kuvuliwa nguo), alitemewa mate, na mwishowe aliuawa,lakini ndiye mkombozi wetu,Naamini Rais Magufuli alikufa akiwa na hakika anakwenda na Bwana Yesu,maana aliimba nyimbo kabla ya kifo chake,,aliwaita Mkuu wa Wakatoliki Kadrinali Pengo,na Mkuu wa Waislam,Mufti alikaa nao kwa ajili ya utakaso wa kiroho,hii ni neema wanaipata wachache na ukiipata basi jua kwamba Mungu alikufanya kuwa mwana na alishakuhesabia haki,hivyo basi atahahakikisha unatakasika kabla ya kwenda kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…