Rozay mbona hajapost waka waka ?

Rozay mbona hajapost waka waka ?

kitalembwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2014
Posts
3,607
Reaction score
9,430
hi jf members,,,,,
Niende direct kwenye mada, ieleweke mimi napenda muziki mzuri haijalishi nani kaimba, kwa maana hiyo sina team Naseeb(diamond) ni msanii mzuri sana vivyo hivyo kwa Ali kiba.

Ni takribani wiki moja imeshapita tangia diamond aachie wimbo wake mpya aliefanya na mwanamuziki wa hip hop anaetokea Miami(USA) Rick Ross, binafsi nilifarijika sana kama mtanzania kwani muziki wetu unapiga hatua kila siku, haikua kazi ndogo kufanya colabo na wasanii wakubwa duniani.

kwanza management zao wanaangalia vitu vingi sana mpaka wakubali kufanya kazi na wewe. baadhi ya vitu wanavyoangalia ni fun base yako kuanzia nchini kwako na nje ya nchi, pia wanaangalia kazi zako ulizotoa na zilivyopokewa, hapa wataangalia pia viewers (u tube/vevo nk).

Pia wanaweza kuangalia baadhi ya tuzo kubwa ulizowahi kushiriki ama kushinda na mwisho kabisa watazingatia kama uliwahi kufanya kolabo na msanii mwingine mkubwa, wakijihirisha yote hayo watakaa na wewe msanii (management yako) na kutangaza dau lao, ukifikia mnafanya kazi.

Kuhusu diamond na rozay nadhani haikua na ugumu mkubwa sana kufanya yote haya, kampuni kubwa na maarufu ya kifaransa (BELAIRE) ambayo wote wana mkataba wa kuitangaza, imeplay part kubwa sana kufanikisha hii collaboration.

Swali, mbona huyu black america hajawahi kupost chochote kuhusiana na hii nyimbo ?walau hata kipande kimoja cha video yao tu, hii kazi imebakia kufanywa na timu ya wcb pekee, jamaa hajatoa sapoti kabisa,kwa nini nasema haya ? au kwa nn pengine rozay alihitaji kupost ? hakuna ubishi jamaa ni mwanamziki mkubwa world wide.

Na anafatiliwa sana kutoka pande tofauti za dunia, kitendo cha kupost kuwa amefanya nyimbo na diamond na kumtag pale ili watu wafatilie link na kuona nyimbo yenyewe kungemwongezea kitu huyu kijana wetu wa tandale hii ni tafsiri gani ?dharau? wamebaki kina babu tale salam raymond na harmo wanapost na tag kibao richforever lakini wapi poleni sana wcb.

Kuna mshirika na mdau mkubwa wa rozay anaefahamika kama black bomaybach alifariki hapa majuzi, fasta diamond naona kapost r.i.p bro, hivi kweli kulikua na ukaribu wa dai na blackbomay kiasi kwamba angempost ? Au jamaa anatafuta ujiko ?
wenye timu yao mnatakuja kuniattack, sina team just nmeamua kushare tu
 
WCB wanachoangalia ni maslah yao binafsi bila kujali wanavyojishusha wala maneno ya watu. Ndo maana kila kukicha wanatengeneza kiki mpya zinazowaweka akilin na midomon mwa watu.

Boss hapangiwi cha kupost ndo msemo unamfaa belaire boss. Atapost akipenda au anaweza asipost kabisa maana colabo tu imefanikiwa kumpa mafanikio dai

Kupost R.I.P haimaanish mpaka uwe na ukaribu na marehemu. Mfano ngwair,kanumba na wengineo, wengi walitoa R.I.P za kutosha wakati hawakua na ukaribu nae.
 
Kujipendekeza kupo kote kwa masikini hata kwa matajiri. Kupata unachohitaji kwa namna moja au nyingine lazima utajipendekeza.
Maskini ataendelea kuwa maskini tu!kwa mawazo haya utaendelea kusindikiza watu duniani;wenzio wanatafuta hela wewe unaita kujipendekeza kweli maskini jeuri
 
Kujipendekeza kupo kote kwa masikini hata kwa matajiri. Kupata unachohitaji kwa namna moja au nyingine lazima utajipendekeza.
Ukiona mtu anamlaumu mtu kwa kujipendekeza kwenye manufaa na kusikoshusha utu wake ujue ataendelea kuwa maskini
 
Kama umebahatika kuangalia behind the scene ya video ya wakawaka, ungemuona black bomay yupo pale. In short sijajua kwa nini wabongo tunatengeneza imagination tu za kufikilika. Hata kumi wish mtu R.I.P mnasema ni kujipendekeza? Wakati huku mtaani tunashiliki mazishi ya watu tusiowafaamu kabisa
 
We nenda account ya Rozay kapost hiyo wimbo wa wakawaka au ufuatilii vizuri,sema mtandao unanizingua ikikaa poa nitappst screenshot umu.
 
Ni kama Tecno alivyoipotezeaga video yake na Madee maana ilikuwa utumbo mtupu . Bado Hallelujah haijapitwa kwa ubora wa audio na video na huu wimbo wa wala waka
 
kijana unatakiwa ujue ya kwamba kuna principle mbili kuu za maisha ili uweze kufanikiwa 1. kujipendekeza 2.kulazimisha. katika kesi hii diamond ndio muhitajia so ni lazima ajipendekeze ili aweze kufanikiwa
 
Ni kweli hajampost hawa wamarekani wana dharau sana, ila hii haijamtokea Diamond tu hata Davido alipofanya collabo na Meek Mill hakuipost wala kumpa support yoyote. Mnyama Drake naonaga ndio anajitahidi kutoa support kwa wasanii wa Africa pamoja na kuwa yuko juu kuliko hao kina Rozay
 
Screenshot_20171213-015307.png
 
WCB wanachoangalia ni maslah yao binafsi bila kujali wanavyojishusha wala maneno ya watu. Ndo maana kila kukicha wanatengeneza kiki mpya zinazowaweka akilin na midomon mwa watu.
Sasa hili linahusiana vipi na mada husika?!
 
Ni kweli hajampost hawa wamarekani wana dharau sana, ila hii haijamtokea Diamond tu hata Davido alipofanya collabo na Meek Mill hakuipost wala kumpa support yoyote. Mnyama Drake naonaga ndio anajitahidi kutoa support kwa wasanii wa Africa pamoja na kuwa yuko juu kuliko hao kina Rozay
Eeeehhh bhna naskia drake yupo kweny list tano bora ya wasanii matajiri duniani
 
Back
Top Bottom