RPC Dodoma atumbuliwa baada ya kutoa taarifa tata ya binti kulawitiwa anaweza kuwa anajiuza

RPC Dodoma atumbuliwa baada ya kutoa taarifa tata ya binti kulawitiwa anaweza kuwa anajiuza

Hiv Afande ni ww kwel? Maana nna muda nkiwa nafuatilia utendaji ngazi ya wilaya akiwa OCD sijui na ulifanya vzur ,hata ulipopata u RPC nlifurai sana ,ila Kwa Hili jaman umekera sana ,,Bora ungelaumiwa kukaa kmya kulko kuongea hayo,alaf nlikua eti najidanganya kua ww ni mcha Mungu sana na huwez potosha haki ya mnyonge '' au basi maana na mm ni kama nimevuta bangi na mlevi
Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie,huyu mama ana roho mbaya sana hata sijui kama ana mume.
 
Hapa kulikuwa na uwezekano wa kulindana na kesi ina public interest kwa sababu suspects ni wanadhaniwa ni kuwa watu wa wizara inayotakiwa kutulinda sisi na mali zetu.Hiyo ya watoto watatu unaweza ukawasilana naye kupitia vyanzo vinavyohusika.
Kati ya Watoto wadogo na huyo dada ni wapi kulitakiwa kuwa na public interest?

Nani hasa alitakiwa kutendewa Haki? Watoto au huyo binti mzoefu?
 
Tumeona taarifa kwenye vyombo vya habari yenye kichwa cha habari kinachosema, "RPC; ANAYEDAIWA KUBAKWA NA KULAWITIWA ALIKUWA KAMA ANAJIUZA", kauli inayodaiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Hayo yametokana na mazungumzo kwa njia ya simu na Mwandishi wa gazeti la Mwananchi ambaye miongoni mwa maswali aliyomuuliza kamanda (mwandishi huyo), Je upelelezi wa kesi umekamilika? na swali lingine alilomuuliza inadaiwa alikuwa anajiuza? Majibu ya kamanda aliyomjibu mwandishi huyo ni kwamba hata kama ni hivyo hangestahili kutendewa hivyo.

Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa kuwa kauli hiyo kama inavyoonekana kwenye hicho kichwa cha habari siyo msimamo wa Jeshi la Polisi kauli sahihi ni kama zilivyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi kwa umma Agosti 4,6 na 9,2024. Vilevile tungependa kujulisha kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakamani leo Agosti 19,2024.

Jeshi la Polisi lingependa kuomba radhi kwa kila mmoja aliyeguswa na kuchukizwa na kauli hiyo inayosambaa kwenye vyombo vya habari wakati ufuatiliaji ukifanyika kupata usahihi wake. Aidha wakati uchunguzi huo wa kupata usahihi wa kauli hizo, Mkuu wa Jeshi la Polisi amefanya mabadiliko madogo kwa kumhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Theopista Mallya kwenda Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP George Katabazi.

View attachment 3073887

Pia soma>> Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza
Mbona alie piga watu na kuongoza wenzake kuiba pesa na simu mmekaa kimya?
Haya ni maigizo..
Tuna taka kusikia IGP na kamishna wake na Waziri wake wamejjongeza na kuguachia ofisi zetu.
 
Huyu mama kazi yake ni Nzuri sana!Ila kwenye hili ulimi umemponza,ulimi kiungo kidogo madhara yake ni makubwa sana.
 
Lakini kasema ukweli
Yule dogo anaonekana alikua ndio kazi yake Ile

Shida ni wale jamaa kumrekodi na kumpiga mande

Inawezekana dogo alielewana na mmoja ila majamaa yakaamua kumkomoa

Mabinti acheni tamaa
Hatutaki kujua kazi ya binti, kama ambavyo hatutaki kujua "kazi" iliyowafikisha wewe na huyo afande huko juu!
 
Sikuhizi napitwa Kuna nn tena
Kuna vijana wanaosadikika kuwa watumishi wa JWTZ, walimteka binti wakamla mande wakarekodi na kusambaza video.....kumekucha na kauli za sintofahamu kutoka Kwa mamlaka za jeshi la police katika kushugulikia jambo hlo
 
ukiwa kiongozi Unapaswa uwe mjanja mjanja sana mwenye kujibu maswali
Maswali mengine ni ya kimtego alafu yanakera.

Ukijiingiza tu huchomoki asee ULIMI umeponza watu sana na ndio mana Misukule inakatwa ulimi inavyosemekana lakini.
 
Nini hasara ya kurudi makao makuu kusoma magezeti?
Mkuu hauelewi maana ya kuwekwa benchi'nini?

Rpc ana cheo na madaraka.

Kurudishwa makao makuu kanyang'anywa madaraka na kubakiwa na cheo.

Au na ufafanuzi huu bado hauelewi faida yake?
 
Taifa si pori wala kichaka.....

Ya baba wa taifa hayati JKN na "kila mtu ANASTAHILI heshima ya KUTAMBULIWA na KUTHAMINIWA UTU wake".

Mama Samia ana utu....

Watanzania silaha yetu ni utu.....

#Nchi Kwanza[emoji7]
#Utu Wa Watanzania [emoji7]
 
Back
Top Bottom