RPC Dodoma atumbuliwa baada ya kutoa taarifa tata ya binti kulawitiwa anaweza kuwa anajiuza

Aliyeelewa mabadiliko yaliyofanywa anielewesha kwa jinsi nilivyosoma mbona huyo RPC ni kama kabadilishiwa tu sehemu ya kazi?🤔
Yes,katolewa tu kwenye ulaji na posho lukuki anaenda soma magazeti
 
Tumeona taarifa kwenye vyombo vya habari yenye kichwa cha habari kinachosema, "RPC; ANAYEDAIWA KUBAKWA NA KULAWITIWA ALIKUWA KAMA ANAJIUZA", kauli inayodaiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Hayo yametokana na mazungumzo kwa njia ya simu na Mwandishi wa gazeti la Mwananchi ambaye miongoni mwa maswali aliyomuuliza kamanda (mwandishi huyo), Je upelelezi wa kesi umekamilika? na swali lingine alilomuuliza inadaiwa alikuwa anajiuza? Majibu ya kamanda aliyomjibu mwandishi huyo ni kwamba hata kama ni hivyo hangestahili kutendewa hivyo.

Pia soma>> Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza

Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa kuwa kauli hiyo kama inavyoonekana kwenye hicho kichwa cha habari siyo msimamo wa Jeshi la Polisi kauli sahihi ni kama zilivyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi kwa umma Agosti 4,6 na 9,2024. Vilevile tungependa kujulisha kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakamani leo Agosti 19,2024.

Jeshi la Polisi lingependa kuomba radhi kwa kila mmoja aliyeguswa na kuchukizwa na kauli hiyo inayosambaa kwenye vyombo vya habari wakati ufuatiliaji ukifanyika kupata usahihi wake. Aidha wakati uchunguzi huo wa kupata usahihi wa kauli hizo, Mkuu wa Jeshi la Polisi amefanya mabadiliko madogo kwa kumhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Theopista Mallya kwenda Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP George Katabazi.

Kuna kitu hakiko sawa kwenye hili jeshi la IGP Wambura. Muda unaongea mengi na yanaanza kusikika. Polisi kuamua kusema alichosema huyo aliyetolewa ni kuwadharau watanzania na kulidhalilisha jeshi la polisi
 
Tumeona taarifa kwenye vyombo vya habari yenye kichwa cha habari kinachosema, "RPC; ANAYEDAIWA KUBAKWA NA KULAWITIWA ALIKUWA KAMA ANAJIUZA", kauli inayodaiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Hayo yametokana na mazungumzo kwa njia ya simu na Mwandishi wa gazeti la Mwananchi ambaye miongoni mwa maswali aliyomuuliza kamanda (mwandishi huyo), Je upelelezi wa kesi umekamilika? na swali lingine alilomuuliza inadaiwa alikuwa anajiuza? Majibu ya kamanda aliyomjibu mwandishi huyo ni kwamba hata kama ni hivyo hangestahili kutendewa hivyo.

Pia soma>> Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza

Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa kuwa kauli hiyo kama inavyoonekana kwenye hicho kichwa cha habari siyo msimamo wa Jeshi la Polisi kauli sahihi ni kama zilivyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi kwa umma Agosti 4,6 na 9,2024. Vilevile tungependa kujulisha kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakamani leo Agosti 19,2024.

Jeshi la Polisi lingependa kuomba radhi kwa kila mmoja aliyeguswa na kuchukizwa na kauli hiyo inayosambaa kwenye vyombo vya habari wakati ufuatiliaji ukifanyika kupata usahihi wake. Aidha wakati uchunguzi huo wa kupata usahihi wa kauli hizo, Mkuu wa Jeshi la Polisi amefanya mabadiliko madogo kwa kumhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Theopista Mallya kwenda Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP George Katabazi.

Kumeozaa
 
Ngoja mama etu akatulie makao makuu ajisomee magazeti pengine akili itamuingia vizuri...
 
RPC aliongea akiwa amelewa!

20240819_140603.jpg
 
Viongozi wenye dhamana ya kuwa wasemaji au wenye majukwaa ya kusemea, wanapaswa kuwa makini na kutafakari vema kabla ya kutoa kauli zao kwa umma. Katikati ya sakata la binti mtajwa, haikupendeza kiongozi kutoa kauli nyepesi na za kubeza tukio zima; ingawa pia makosa ya bangi, kujiuza na hata kurusha picha chafu mitandaoni bado yanahojika kisheria. Hii haina tofauti na yule aliyezungumzia kuiba kura wakati anajua Bosi wake anapambana kurejesha maelewano (harmony) ya kitaifa..!
 
Nice move jeshi la polisi limejaa genge la wahauni na mambo machafu waache kulindana walinde raia na haki zao

Tunasubiria huyo afande wamtaje aliohusika na ubakaji.
 
1. Hivi "Malaya" anapoteza haki zake kama raia?

2. Kimsingi umalaya (chovya chovya) ni sehemu ya tamaduni zetu huku Tanganyika -nadra kukuta mtu mwenye mapenzi mmoja, hivyo tukae kwa tahadhari hali ni mbaya.
 
Attachments

  • cf533c75e95441ab8b37eb34bd72a716_455728847_18348873718189072_3131131201557665363_n.jpg
    cf533c75e95441ab8b37eb34bd72a716_455728847_18348873718189072_3131131201557665363_n.jpg
    131.3 KB · Views: 2
Back
Top Bottom