RPC Jongo: Msikubali kukamatwa na askari asiye na kitambulisho

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
83,659
Reaction score
90,151
Jeshi la Polisi mkoani Geita limewataka wananchi kutokubali kukamatwa na mtu yeyote anayedai kuwa askari polisi bila kuonyesha kitambulisho na kueleza kituo gani alichotokea.

1744182979031.png

Kamanda wa Polisi humo, Safia Jongo ametoa kauli hiyo Aprili 9, 2025 wakati wa mafunzo ya ulinzi shirikishi na polisi jamii, yaliyotolewa kwa watendaji wa kata, vijiji, mitaa, wenye viti na maofisa tarafa, yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) kwa lengo la kuimarisha usalama wa wananchi kupitia ushirikiano wa karibu.

Amesema kumekuwa na matukio ya utekaji, yanayodaiwa kufanywa na watu waliovaa sare za polisi, wakiwa kwenye magari yanayodaiwa kuwa ya Serikali, lakini hawatoi uthibitisho wowote kwa wananchi jambo linalotia hofu na kuathiri imani kwa vyombo vya dola.

"Askari wa kweli anapokwenda kukamata mtu lazima ajitambulishe kwa jina, awe na kitambulisho cha kazi na aseme anatoka kituo gani. Kama hana hivyo, huyo si askari ni mtu wa kawaida ambaye anaweza kuwa jambazi au mhalifu," amesema Safia.
 
Mimi siyo kitambulisho tu! Si unaweza kukitengeneza stationery! Askari akija, aanzie kwanza kwa kiongozi wangu wa mtaa. Aseme na sababu ya kunikamata. Na pia lazima nimjulishe kwanza jamaa yangu ambaye ni wakili msomi, kwa ajili ya mwongozo.

Kinyume na hapo, tutapambama kwa kweli. Kwa sababu sitakubali kirahisi tu kuingia kwenye hari lako jeupe, na lililofichwa namba zake za usajili.
 
Jeshi la Polisi mkoani Geita limewataka wananchi kutokubali kukamatwa na mtu yeyote anayedai kuwa askari polisi bila kuonyesha kitambulisho na kueleza kituo gani alichotokea.

Kamanda wa Polisi humo, Safia Jongo ametoa kauli hiyo Aprili 9, 2025 wakati wa mafunzo ya ulinzi shirikishi na polisi jamii, yaliyotolewa kwa watendaji wa kata, vijiji, mitaa, wenye viti na maofisa tarafa, yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) kwa lengo la kuimarisha usalama wa wananchi kupitia ushirikiano wa karibu.

Amesema kumekuwa na matukio ya utekaji, yanayodaiwa kufanywa na watu waliovaa sare za polisi, wakiwa kwenye magari yanayodaiwa kuwa ya Serikali, lakini hawatoi uthibitisho wowote kwa wananchi jambo linalotia hofu na kuathiri imani kwa vyombo vya dola.

"Askari wa kweli anapokwenda kukamata mtu lazima ajitambulishe kwa jina, awe na kitambulisho cha kazi na aseme anatoka kituo gani. Kama hana hivyo, huyo si askari ni mtu wa kawaida ambaye anaweza kuwa jambazi au mhalifu," amesema Safia.
Ajiandae kupelekwa makao makuu kusoma magazeti.
 
nasubiria kile ki press release cha msemaji wao yule mchagga full typing error yaani huyo akisavaivu hadi wiki ijayo mniite umbwa nimekaa pale,
 
Jeshi la Polisi mkoani Geita limewataka wananchi kutokubali kukamatwa na mtu yeyote anayedai kuwa askari polisi bila kuonyesha kitambulisho na kueleza kituo gani alichotokea.

Kamanda wa Polisi humo, Safia Jongo ametoa kauli hiyo Aprili 8, 2025 wakati wa mafunzo ya ulinzi shirikishi na polisi jamii, yaliyotolewa kwa watendaji wa kata, vijiji, mitaa, wenye viti na maofisa tarafa, yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) kwa lengo la kuimarisha usalama wa wananchi kupitia ushirikiano wa karibu.

Amesema kumekuwa na matukio ya utekaji, yanayodaiwa kufanywa na watu waliovaa sare za polisi, wakiwa kwenye magari yanayodaiwa kuwa ya Serikali, lakini hawatoi uthibitisho wowote kwa wananchi jambo linalotia hofu na kuathiri imani kwa vyombo vya dola.

“Askari wa kweli anapokwenda kukamata mtu lazima ajitambulishe kwa jina, awe na kitambulisho cha kazi na aseme anatoka kituo gani. Kama hana hivyo, huyo si askari ni mtu wa kawaida ambaye anaweza kuwa jambazi au mhalifu,” amesema Safia.

Video: EATV
 
NI sawa na kusema:

"Ni lazima watu wote wafunge mikanda kwenye daladala"

Halitelelezeki! Hata yeye hatekelezi!
 
Back
Top Bottom