Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara limetoa ufafanuzi juu ya madai ya Polisi kuwatumia Mgambo katika shughuli zao
Awali, Mwanachama wa JamiiForums.com alidai Mgambo hao wamekuwa wakitumiwa usaidia shughuli za Kipolisi wamekuwa hawatendi haki kwa baadhi ya Wananchi pia akadai wanashirikiana na Whalifu wengine kufanya uhalifu.
Hoja ya Mdau hii hapa ~ OCD Bunda fanya uchunguzi wa kina juu ya mgambo wako, wanashirikiana na vibaka
Ufafanuzi wa Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Mara, ACP Salim Morcase:
Siamini katika hayo madai ya huyo Mwananchi, kwa sababu simu yangu ni simu ya wananchi wote, kama angekuwa na jambo angenipigia kama ninavyopigiwa simu na Wananchi wengine.
Tuna weledi wa kutosha, tuna Askari wengi, shughuli zetu zote tunasimamia wenyewe. Yameshatoka maelekezo mbalimbali ya viongozi wetu, Jeshi la Polisi lipo vizuri kiweledi, hatutumii Mgambo yeyote, narudia hatutumii Mgambo yeyote kutekeleza majukumu yetu.
Shughuli zetu tunasimamia wenyewe, hao wanaojiita Magambo wanajipanga kazi wenyewe na ni sehemu ya Wahalifu kama walivyo wahalifu wengine.
Mwananchi yeyote kama ana jambo la ufafanuzi namba yangu ipo hewani, hata hapa ninavyoongea na wewe (Mei 5, 2024) nipo katika ukaguzi wa kata kwa kata, jambo hilo nikilipata na kuwabani wahusika hatua zitachukuliwa