DNA kukutwa kwenye nguo au gari siyo shida sababu wawili hao ni wapenzi. Pia kukuta kwamba ni kweli bint aliingiliwa kinyume nayo siyo shida, tatizo ni je, aliingiliwa na nani? Sababu vipimo havikufanywa wakati ule, bali kama vimefanyika basi ni jana, yaani nearly 2 weeks later.
Hivyo ushahidi wa uwepo wa DNA za bint kwenye nguo au gari siyo issue sababu Kinachotafitwa siyo uthibisho kama wawili hawa wana mahusiano au wamewahi kiwa pamoja eneo lile, bali ni kinachotafutwa ni kama Nawanda alimuingilia kinyume na maumbile.