Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Natoa ombi hili kwako maana wewe umekabidhiwa jukumu hili la kulinda usalama wa raia na mali zao kama kamanda wa mkoa.
Tukio hili baya lilitokea tar 26/10/2019 ndani ya ofisi ya kata ya Kahama wilaya ya ilemela Mkoa wa Mwanza. Watuhumiwa waliteswa na Mwanajeshi na Migambo kwa idhini ya Mtendaji wa kata na Mwenyekiti. Nzengo nzima iliona tukio hili na mmoja wa watuhumiwa akijulikana Omela alifariki.
Sasa imepita miezi mitatu hakuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa. Watu waliofanya tukio hili wapo wanatamba mitaani tu.
Mke wa marehemu alifuatilia hadi kwa mkuu wa wilaya. DAS akampigia simu OCD Ilemela amsaidie ili wahusike wakamatwe lakini majibu aliyopata ni kuwa marehemu alikuwa jambazi na alipigwa na wananchi. Pia watafanya uchunguzi.
Kama alikuwa jambazi na alipigwa na wananchi wenye hasira kali tena kwenye mji wa watu.
Sasa kwa sababu kujichukulia sheria mkononi ni kosa hao, waliomuua mtuhumiwa wakamatwe. Mbona RPC mkoa magharibi Unguja alichukua hatua kwa askari aliyemuacha mtuhumiwa auliwe na wananchi wenye hasira kali na nini kinafanya hatua zisichukuliwe huko Mwanza.
N.B: Tanzania ni nchi yenye kufuata misingi ya sheria na utawala bora.Ibara ya katiba ya JMT 13(6) imeweka wazi jinsi haki watuhumiwa zinatakiwa kulindwa. Mahakama ndio chombo pekee cha kuwatia hatiani watuhumiwa.