RPC wa Dodoma, Afande Muroto aituhumu JamiiForums kwa kupotosha taarifa za kifo cha Sheikh Rashid Bura

Mkuu anayempinga Murotto siyo jf , ni familia ya marehemu , mtu aliyekufa kwa shinikizo la damu anakuwaje na majeraha manne makubwa kwenye mwili wake ? Hawa polisi ndio waliosema Mwangosi alitupiwa kitu chenye ncha kali na wafuasi wa chadema , uliamini hilo ?

Halafu lingine ni hili , JF haitofanya kazi zake kwa kufuata maelekezo ya Murotto au mtu mwingine yeyote ukiwemo wewe ( hili ni onyo )
 
MOYO ULIFELI KWANI ALIFANYA MTIHANI WA DARASA LA NGAPI? ALISHINDWA HATA KUPATA FEKI AKAIBIA? MITIHANI KWELI YAWEZA KUWA KITU MBAYA KABISA, SIJUI WATALITUHUMU BARAZA LA MAPEPA KWA KIFO CHAKE?
Shule za kata bwana ! Ku-fail ( kufeli) ni ktk kufanya mitihani tu!
 
Lakini kinachonishangaza ni hiki:

Polisi Tanzania wanao utaalam wa kujua kilichosababisha kifo na kukitangaza?

Au maiti ilishafanyiwa uchunguzi na wataalam husika, na huko ndiko alikotoa taarifa hiyo?

Je, yeye ndie mwenye mamlaka ya kutoa taarifa hiyo?

Ndugu wa marehemu hawakushirikishwa katika uchunguzi uliofanyika? Kwa maana wangeshirikishwa pasingekuwepo na sintofahamu kutoka kwao.

Mimi nadhani kuna umhimu mkubwa kwa Tanzania kurudi kwenye taratibu zinazotambulika katika kufanya mambo kama haya.
Polisi hawezi kujisemea tu chochote anachoona inafaa kisemwe.
 
Mkuu JokaKuu penye ukweli uwongo hujitenga........

Hao Polisi wamezoea kutulisha matango pori, hivi sasa wananchi wameishiwa "appetite" ya kuyatafuna hayo matango pori yao, ndiyo kisa cha povu lote hilo linalowatoka!
 
Kalamu1,
Naunga mkono hoja, kunapotokea kifo chochote cha utata, ndugu wa marehemu lazima washirikishwe kwenye post mortem na kupewa copy ya report kama kuna issue yoyote ya kipolisi kuhitaji forensic investigation ndipo polisi hueleza. Lakini hapa inaelekea ndugu hawajashirikishwa, RPC sio authority wa kueleza siri za mgonjwa ni daktari na familia!.
P
 
No Pasco ni yule yule, juzi, jana na leo, tatizo ni wasomaji wangu siku nikiponda ndio naelezwa kurudi kwenye ubora, siku nikisifu, natafuta u DC!.
Tuwe wakweli, mazuri tusifu, mabaya tukosoe.
P
Kinachowashinda watanzania wengi ni "kusoma na kuelewa"
 
Eeeeh si mchezo aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…