RPC wa Dodoma, Afande Muroto aituhumu JamiiForums kwa kupotosha taarifa za kifo cha Sheikh Rashid Bura

RPC wa Dodoma, Afande Muroto aituhumu JamiiForums kwa kupotosha taarifa za kifo cha Sheikh Rashid Bura

JF wanaendekeza habari za uzushi kwa kisingizio cha “user generated content”, cha kushangaza yoyote atakayeleta habari ya uzushi hatapewa adhabu kali, kwa mwendo huu JF inaenda kuwa kijiwe cha uzushi na propaganda na sio mahali salama pa kuhabarika.
Mkuu anayempinga Murotto siyo jf , ni familia ya marehemu , mtu aliyekufa kwa shinikizo la damu anakuwaje na majeraha manne makubwa kwenye mwili wake ? Hawa polisi ndio waliosema Mwangosi alitupiwa kitu chenye ncha kali na wafuasi wa chadema , uliamini hilo ?

Halafu lingine ni hili , JF haitofanya kazi zake kwa kufuata maelekezo ya Murotto au mtu mwingine yeyote ukiwemo wewe ( hili ni onyo )
 
Hivi huu Uongo mtaacha lini_  Unawaambia nini Jeshi la Polisi Tanzania  Toa maon ( 648 X 640 ).jpg

Natoa wito kwa IGP Sirro kuchukua maamuzi magumu ili kulinda heshima ya jeshi la polisi.

Kifo hiki kina walakini, vinginevyo familia ya marehemu itatokomezwa ili kuficha ushahidi.
 
Hapa ndio Muroto anapo angukia pua. Kijana wa marehemu amekataa version ya Muroto na kusisitiza kuwa mwili wa Mzee wake ulikutwa hauna nguo na una dalili ya majeraha. Lbda kama nae amezushiwa kusema hivyo, vinginevyo taarifa ya polisi ina walakini na JF ina msingi wa kuleta taarifa iliyoletwa.
Nafikiri jeshi letu la polisi kwenye uwazi na ukweli (in Mkapa's voice) wana matatizo makubwa hadi wanafungua kesi ambazo hazipo, wanatoa reporti ambazo si sawa.
Lakini kinachonishangaza ni hiki:

Polisi Tanzania wanao utaalam wa kujua kilichosababisha kifo na kukitangaza?

Au maiti ilishafanyiwa uchunguzi na wataalam husika, na huko ndiko alikotoa taarifa hiyo?

Je, yeye ndie mwenye mamlaka ya kutoa taarifa hiyo?

Ndugu wa marehemu hawakushirikishwa katika uchunguzi uliofanyika? Kwa maana wangeshirikishwa pasingekuwepo na sintofahamu kutoka kwao.

Mimi nadhani kuna umhimu mkubwa kwa Tanzania kurudi kwenye taratibu zinazotambulika katika kufanya mambo kama haya.
Polisi hawezi kujisemea tu chochote anachoona inafaa kisemwe.
 
Mkuu JokaKuu penye ukweli uwongo hujitenga........

Hao Polisi wamezoea kutulisha matango pori, hivi sasa wananchi wameishiwa "appetite" ya kuyatafuna hayo matango pori yao, ndiyo kisa cha povu lote hilo linalowatoka!
 
Kalamu1,
Naunga mkono hoja, kunapotokea kifo chochote cha utata, ndugu wa marehemu lazima washirikishwe kwenye post mortem na kupewa copy ya report kama kuna issue yoyote ya kipolisi kuhitaji forensic investigation ndipo polisi hueleza. Lakini hapa inaelekea ndugu hawajashirikishwa, RPC sio authority wa kueleza siri za mgonjwa ni daktari na familia!.
P
 
1. Aliwahi fanyakazi ofisi ya CAG

2. Anahusika kayika taasis ya Dalai Islamic center ambayo hata CAG mstaafu yupo

3. Kabla ya kifo alikuwa safaarini kuhudhuria kwenye kikao cha tasisi yao ambacho CAG mstaafu alikuwepo ambae nae ilisemekana alitekwa baada ya kutoka kwenye kikao hicho

Sent using Jamii Forums mobile app
Eeeeh si mchezo aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom