Polisi Tanzania wanao utaalam wa kujua kilichosababisha kifo na kukitangaza?
Kazi hiyo popote pale duniani inafanywa na Watalaam wa afya. Ndiyo maana kuna kitu kinaitwa ''Forensic examination inayofanywa kwa utaalam wa Pathology''
Au maiti ilishafanyiwa uchunguzi na wataalam husika, na huko ndiko alikotoa taarifa hiyo?
Inawezeakana ilifanyika, katika mass communication hilo lilitakiwa liwe wazi
Je, yeye ndie mwenye mamlaka ya kutoa taarifa hiyo?
Taarifa anaitoa kwa kushirikiana na Dr na Wanafamilia. Hawa ni mashahidi wa post mortem.
Ndugu wa marehemu hawakushirikishwa katika uchunguzi uliofanyika?
Kwa maana wangeshirikishwa pasingekuwepo na sintofahamu kutoka kwao.
Kisheria wanapaswa kushirikishwa katika uchunguzi. Sijui kama hilo lilifanyika, na kama lilifanyika mkanganyiko unatoka wapi? Na kwanini Kamanda hakueleza?
Mimi nadhani kuna umhimu mkubwa kwa Tanzania kurudi kwenye taratibu zinazotambulika katika kufanya mambo kama haya.
Polisi hawezi kujisemea tu chochote anachoona inafaa kisemwe.
Ndiyo maana nasema kisheria Kamanda ameliweka jeshi pagumu sana.
Shahidi wa post mortem si Polisi, ni Daktari na huyu ndiye anaweza kusimama mahakamani kutoa taarifa za kitaalam. Kwa maelezo ya Kamanda, yeye ndiye shahidi na hapo kuna tatizo
Lakini pia kutangaza kifo na kutangaza sababu za kifo ni mambo ya faragha hadi pale next of kin au huku kwetu Tanzania Mwakilishi wa Familia atoe idhini hiyo.
Je, kulikuwa na Idhini ya Familia, kwanza, kutangaza kifo na pili kutoa sababu za kifo?
Ilitakiwa Kamanda asimame na watu hao, Dr na MwanaFamilia ili taarifa yake ikamilike isiache shaka wala mawaa. Kilichotokea kimeharibu kuliko kutengeneza.
Maelezo ya Kamanda yanazidisha ''conspiracy theory'' hata kama ni natural death.
Nadhani hakushauriwa vizuri kuhusu hili. Laiti tungekuwa na mfumo wa private investigator, Kamanda angekuwa katika nafasi ngumu sana kisheria.