RPC wa Dodoma, Afande Muroto aituhumu JamiiForums kwa kupotosha taarifa za kifo cha Sheikh Rashid Bura

RPC wa Dodoma, Afande Muroto aituhumu JamiiForums kwa kupotosha taarifa za kifo cha Sheikh Rashid Bura

Pascal Mayalla,
Kama usemayo Pascal ni kweli kwamba Assad na Rashid walikuwa kwenye mkutano mmoja basi kuna tatizo pahala na Zitto akamatwe na kuhojiwa.

Tarehe 25/12/2019 Assad kapotea na mwili wa shehe kupatikana? Isijekuwa ni siasa za maruhani hizi!
 
Polisi Tanzania wanao utaalam wa kujua kilichosababisha kifo na kukitangaza?
Kazi hiyo popote pale duniani inafanywa na Watalaam wa afya. Ndiyo maana kuna kitu kinaitwa ''Forensic examination inayofanywa kwa utaalam wa Pathology''
Au maiti ilishafanyiwa uchunguzi na wataalam husika, na huko ndiko alikotoa taarifa hiyo?
Inawezeakana ilifanyika, katika mass communication hilo lilitakiwa liwe wazi
Je, yeye ndie mwenye mamlaka ya kutoa taarifa hiyo?
Taarifa anaitoa kwa kushirikiana na Dr na Wanafamilia. Hawa ni mashahidi wa post mortem.
Ndugu wa marehemu hawakushirikishwa katika uchunguzi uliofanyika?
Kwa maana wangeshirikishwa pasingekuwepo na sintofahamu kutoka kwao.
Kisheria wanapaswa kushirikishwa katika uchunguzi. Sijui kama hilo lilifanyika, na kama lilifanyika mkanganyiko unatoka wapi? Na kwanini Kamanda hakueleza?

Mimi nadhani kuna umhimu mkubwa kwa Tanzania kurudi kwenye taratibu zinazotambulika katika kufanya mambo kama haya.
Polisi hawezi kujisemea tu chochote anachoona inafaa kisemwe.
Ndiyo maana nasema kisheria Kamanda ameliweka jeshi pagumu sana.

Shahidi wa post mortem si Polisi, ni Daktari na huyu ndiye anaweza kusimama mahakamani kutoa taarifa za kitaalam. Kwa maelezo ya Kamanda, yeye ndiye shahidi na hapo kuna tatizo

Lakini pia kutangaza kifo na kutangaza sababu za kifo ni mambo ya faragha hadi pale next of kin au huku kwetu Tanzania Mwakilishi wa Familia atoe idhini hiyo.

Je, kulikuwa na Idhini ya Familia, kwanza, kutangaza kifo na pili kutoa sababu za kifo?

Ilitakiwa Kamanda asimame na watu hao, Dr na MwanaFamilia ili taarifa yake ikamilike isiache shaka wala mawaa. Kilichotokea kimeharibu kuliko kutengeneza.

Maelezo ya Kamanda yanazidisha ''conspiracy theory'' hata kama ni natural death.

Nadhani hakushauriwa vizuri kuhusu hili. Laiti tungekuwa na mfumo wa private investigator, Kamanda angekuwa katika nafasi ngumu sana kisheria.
 
Pascal Mayalla,
Kama usemayo Pascal ni kweli kwamba Assad na Rashid walikuwa kwenye mkutano mmoja basi kuna tatizo pahala na Zitto akamatwe na kuhojiwa.

Tarehe 25/12/2019 Assad kapotea na mwili wa shehe kupatikana? Isijekuwa ni siasa za maruhani hizi!
Sijasema ni for sure, nimesema nahisi tuu, kwasababu marehemu alikuja Dar kwenye mkutano, haulitajwa ni mkutano gani wa nini na ulifanyika wapi ila miongoni mwa shughuli zake ni kuongoza Taasisi ya dini ya kuwapeleka watu kuhiji Mecca.

CAG Prof. Assad yeye alialikwa kutoa mada kwenye mkutano ule, Prof. Asad aliutaja mkutano ule ni wa nini na ulifanyika wapi. Bado hatuja thibitishiwa marehemu alihudhuria mkutano gani, tukiisha thibitisha hilo ndipo kazi ya connecting the dots ianze, saa hizi bado ni mapema sana.
P
 
HIVI MNAJUA KUWA MUROTO NDIYE RPC BORA WA MAGU. ..

BAADA YA MUROTO NI MAMBOSASA.. . WANAFANYA KAZI NZURI SANA MBELE YA AMIRI JESHI...

SIRRO HAWEZI KUWAFANYA KITU OOTE HAO.. . NA WAO WANA UWEZO WA KUMVIMBIA SIRRO. .. KWA SABABU RAIS YUPO NYUMA YAO.. .
 
Mkuu Pascal Mayalla naona umeanza kurejea kwenye ubora wako!

No Pasco ni yule yule, juzi, jana na leo, tatizo ni wasomaji wangu siku nikiponda ndio naelezwa kurudi kwenye ubora, siku nikisifu, natafuta u DC!.
Tuwe wakweli, mazuri tusifu, mabaya tukosoe.
P
Nakusoma Pascal, unadhani Mystery amekosea kuliweka hivyo? Sisi ni binadamu kuna wakati huteleza. Tatizo la juzi sio kusifu bali ulimpa sifa asiyestahili bahati mbaya kama ujuavyo naye ana wapinzani wakutosha. Ndio maana wengine tunasema mahaba [yakizidi] hupofusha. Umesema "Tuwe wakweli, mazuri tusifu, mabaya tukosoe", nakubaliana nawe lakini kwenye ule uzi mazuri yale hayakuwa ya yule uliempa pongezi kana kwamba yeye ndiye aliye yaleta (causal attribution).
 
Nijuavyo mimi kwa Tanzania ninayoijua haya yote ni upepo tu (credit kwa mzee kikwete) yatapita na tutaendelea na maisha yetu yaleyale kama kawaida. Mpaka hapo upepo mwingine utakapo vuma (tukio lingine litakapotukia) ndiyo tutarudi hapa tena kujadiri kama hivi. Tanzania raha sana!!
 
Mkuu anayempinga Murotto siyo jf , ni familia ya marehemu , mtu aliyekufa kwa shinikizo la damu anakuwaje na majeraha manne makubwa kwenye mwili wake ? Hawa polisi ndio waliosema Mwangosi alitupiwa kitu chenye ncha kali na wafuasi wa chadema , uliamini hilo ?

Halafu lingine ni hili , JF haitofanya kazi zake kwa kufuata maelekezo ya Murotto au mtu mwingine yeyote ukiwemo wewe ( hili ni onyo )
Una akili nyingi na uelewa mpana
 
Taarifa za jeshi la Polisi nchini kuhusu vifo vyenye utata huwa siku zote zinaleta utata zaidi (maswali) badala ya majibu.

Wakati wa kifo cha Mchungaji Mtikila, jeshi la Polisi mkoa wa Pwani lilihitimisha uchunguzi baada ya siku 3 tu kuwa chanzo cha kifo ni kuvunjika kwa mbavu 8 za mchungaji kulikosababishwa na mchungaji kutovaa mkanda wa gari na akatupwa nje kwa kugonga kioo cha mbele na kisha gari likamwangukia. Likaibua maswali yafuatayo


Mjane wa marehemu akalia na kuiomba serikali ifanye uchunguzi zaidi akajibiwa kuwa faili limekwishafungwa. Mpaka leo hakuna ripoti iliyotoka zaidi ya ile iliyotolewa na RPC Pwani.
 
Back
Top Bottom