Kwani Kuna KATIBA mpya imeandikwa au Sheria imetungwa inayoruhusu RPC kuelekeza vijana wake kuhukumu mtu KIFO bila Kumfikiaha Mahakamani akiwa amefungwa pingu akiwa mikononi mwa POLISI???Taarifa mpya kutoka Mkoani Mara zinadokeza kwamba , baada ya sarakasi za kuuawa kwa walioitwa majambazi huko Serengeti , ambapo wadau mbali mbali wamejitokeza kuhoji uhalali wa mauaji hayo ya kishamba , eti leo wameonekana madereva wa bodaboda wakimpongeza RPC Kwa kuua Majambazi , inakadiliwa kuwa Bodaboda zaidi ya 100 walishiriki maandamano hayo ya pongezi ! (Nani atathibitisha kama waandamanaji hao ni madereva wa bodaboda ?) , acha iwe siri.
Bali Mashaka juu ya Jambo hili ni BAADA YA WAONA MBALI KUTAMBUA KWAMBA KUMBE MUANDAAJI WA MAANDAMANO HAYO NI RPC MWENYEWE ! yaani kaandaa kupongezwa ili asitumbuliwe ! haya ndio maajabu ya Tanzania , kama waliouawa ni majambazi hofu ya kutengeneza maandamano ya mchongo inatoka wapi ?
Swali : Hivi ni wapi mlikowahi kukuta bodaboda wanaandamana ili kupongeza mauaji ya majambazi ? Kwanini leo iwe Mkoa wa Mara ? Na je kama hilo jambo limegusa Mkoa wote kwanini yasingeitishwa maandamano ya wananchi wote wa Mara badala ya kikundi kinachoitwa Madereva wa bodaboda ?
KILA UBAYA UTALIPWA
Mbona hili Ombwe la Uongozi linazidi kukua?!!!!!!!