Ni kweli mkuu, first half tuliwapa UHURU ULIOPITILIZA wa kuja golini kwetu.
Mimi sijaumizwa na matokeo, ila namna tulivyocheza hasa first half ndio shida naiona.
Anyways naamini mechi zetu mbili za nyumbani tutashinda na kufikisha pointi 10, lakini hii approach ya leo watu wa ufundi wanatakiwa waitazame upya.
Haka kaujinga ka kutaka kupaki basi ndio kalikowaponza Kaizer Chiefs ile mechi yao dhidi yetu kwa Mkapa, bahati mbaya tu kuna magoli tulikosa ila nne zilikua zinarudi.
Huwezi kupaki basi kuanzia dakika ya kwanza utegemee utafanya hivyo kwa dakika zote tisini, ni kazi mno.
Muonyeshe mpinzani kwamba nawewe ni threat kwake ili aje kukushambulia kwa tahadhari.