RSM (Regimental Sergeant Major) wa Jeshi la Wananchi - JWTZ

RSM (Regimental Sergeant Major) wa Jeshi la Wananchi - JWTZ

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
RSM / Regimental Sergeant Major.

Kwa waliopitia JKT watakuwa wanajua uzito wa askari mwenye mamlaka ya RSM wa kikosi.

Kwa kawaida RSM ni askari mwenye cheo cha Warrant Officer II, au Warrant Officer I, ktk kikosi husika.

RSM hushughulikia masuala ya utii wa askari wa ngazi za chini kikosini, kusimamia mafunzo, usafi, n.k.

Kwa wale tuliopitia JKT tunawakumbuka ma-RSM kama askari mtiifu, mweledi, masafi, makakamavu, makali, mwenye kiherehere, kuzidi askari wote kikosini.

JWTZ pamoja na kuwa na CDF, CoS, na maofisa wengine wa ngazi za juu, linaye askari mwenye mamlaka ya RSM wa jeshi.

Pamoja na kuwatambua maofisa mbalimbali wa JWTZ nimeona leo JF tutambue uwepo wa RSM wa JWTZ.

Warrant Office I Martin Kazilo RSM wa JWTZ anaonekana hapo ktk video kuanzia dakika 59:52.

 
Msimamizi wa nidhamu sio kwa askari wadogo tu,hata maofisa wadogo,ndiye mlezi wa kambi nzima na familia za askari kambini.
Ndiye mtu anayebaki na familia za askari kambini askari wa kikosi wanapokuwa vitani.

Kifupi RSM na mkuu wa kambi ni dugu moja,kasoro vyeo.
 
Msimamizi wa nidhamu sio kwa askari wadogo tu,hata maofisa wadogo,ndiye mlezi wa kambi nzima na familia za askari kambini.
Ndiye mtu anayebaki na familia za askari kambini askari wa kikosi wanapokuwa vitani.

Kifupi RSM na mkuu wa kambi ni dugu moja,kasoro vyeo.

..huyu afande amefafanua vizuri majukumu ya RSM.

 
..hapo chini ni gwaride la miaka 60 ya uhuru.

..kuna utambulisho umefanyika kuhusu wasimamizi wa gwaride na kuna maveteran wa magwaride Tz ambao wameshiriki.

..mmojawapo na parade commander ktk maadhimisho mengi hapa nchini Brigedia Jenerali mstaafu Ambrose Peter Bayeke.

..pia kuna RSM mstaafu wa Jwtz Warrant Office I Faustine Madasha, na RSM wa Jwtz Warrant Office I Peter Kaziro.

..miaka ya nyuma alikuwepo parade RSM maarufu sana Warrant Office I Wilbard Mukama sikumsikia akitajwa.

..Waliiongoza gwaride la Uhuru ni Parade Commander Lt.Col.Himidi Alawi Nguzo; Parade 2-I-C Major.Mboka Nisile Mwangama; Parade Adjutant Capt.Godfrey Matete Malima; Parade RSM Warrant Officer I James Mataba Manumbu.




cc Nguruvi3
 
Nina swali wakuu,hivi ukitoa tattoo hizi alama zingine Kama za tetekuwanga(pox) au black dots kwenye miguu mfano je itafaa?
 
RSM Mundeba 821 KJ alikuwa anatudiss Sana sisi Mujibu wa sheria eti kuruti una hot kama panzi😂 siku nyingi zimepita sijui bado yupo kikosini ilikuwa OP miaka 50 ya JKT 2013
 
Back
Top Bottom