Ruangwa kama Chato

Ruangwa kama Chato

Hii ni kama hadithi ya mwizi au fisadi. Mzazi akiwa mwizi/fisadi akaipa familia raha watamtetea kwa nguvu zoteee... subiri sasa ea mwingine awe mwizi/ fisadi. Utasikia ua, funga, peleka ICC nk. Hii sio hulka njema kabisa.

Sent from my SM-N986B using JamiiForums mobile app
 
Wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015 , sisi Watu wa Kyela tuliokuwa tunampinga Mwakyembe (Aliyetajwa kama PM ajaye) Tulishambuliwa vibaya mno.

Binafsi nimefuatwa inbox na zaidi ya watu10 ili nisimpinge Mwakyembe maana akiwa Waziri Mkuu Kyela yetu ingekuwa Paradiso , Hata hivyo Mwakyembe alipewa ushindi wa mabavu na alipokosa U PM Kyela yote iliripuka kwa furaha (sijui kwanini) .

Nadhani haya ya Ruangwa ndio niliyokuwa naambiwa inbox na wadau .
Jamaa wa ruangwa kajijengea kamtandao ka upigaji sana
 
Waziri Mkuu Majaliwa hana tofauti kubwa na marehemu Magufuli kila mara yuko nyumbani kwao Ruangwa na ni kupeleka miradi kila baada ya miezi kadhaa.

Hajui yeye ni Waziri Mkuu wa nchi nzima? Leo ametoa mikopo Milioni 256, hii hela ni nyingi sana kwa wilaya moja.

Bado nradi wa maji sijui nafikiri Bilioni 500. Kwanini haya mambo ya upendeleo na ubaguzi yameanza wakati wa Magufuli?

Nchi hii haikuwa na mawaziri wakuu kabla? Haya ni matumizi mabaya ya nafasi.

Lini atatembelea wilaya zingine na kupelekea neema ya miradi inayofanana na ambayo amekuwa akiipeleka Ruangwa kila mara?

Amesahau yeye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Atumikie watanzania wote kwa usawa.
Wameanzia Chato,sasa Ruangwa itakwenda mpk nchi yote itajengwa,taratibu mkuu watafika tu na huko uliko,vuta subira,acha wivu mkuu au tukupe wewe u PM tuone jinsi utakavyokwenda kujenga kwa wenzako na uache kwako....
 
Kama hiyo miradi inaenda kuinufaisha Lindi basi sioni shida,nachukia sana mnavyotucheka kwamba hatujapiga hatua;ila kaeni mkijua kwamba hata hatua mliopiga katika mikoa yenu ilitokana na jitihada ya viongozi wa serikali(ndugu zenu) kuelekeza kila mradi wa maendeleo katika mikoa yenu na wakatuacha sisi wanakusini,hapo kabla, kila jambo zuri lilielekezwa sijui Dodoma,Arusha mara shinyanga..

Tawala zilizopita zilikuwa za hovyo sana maana zilijawa na unyumbani,nasi utanzania.

Acheni nasi wanalindi tufaidi maana hii nchi sio ya baba yenu bali ni yetu sote.[emoji57]
Mtaemdelea kuletewa viuatilifu vya magumashi hadi mtaakapo pata uelewa
 
Mkuu acha tu wajenge kwao,nipo Butiama jioni hii,nimetoka kumuagiza boda maziwa mtindi boda kaniambia huwezi kupata,nimeenda mwenyewe kutafuta,Hakuna duka linalouza mtindi butiama.Naongelea maziwa mtindi guys,Butiama inasikitisha sana.Acha viongozi wajenge kwao.
Mbona tunaambiwa huko watu wanafuga sana Ng'ombe?
 
Kama hiyo miradi inaenda kuinufaisha Lindi basi sioni shida,nachukia sana mnavyotucheka kwamba hatujapiga hatua;ila kaeni mkijua kwamba hata hatua mliopiga katika mikoa yenu ilitokana na jitihada ya viongozi wa serikali(ndugu zenu) kuelekeza kila mradi wa maendeleo katika mikoa yenu na wakatuacha sisi wanakusini,hapo kabla, kila jambo zuri lilielekezwa sijui Dodoma,Arusha mara shinyanga..

Tawala zilizopita zilikuwa za hovyo sana maana zilijawa na unyumbani,nasi utanzania.

Acheni nasi wanalindi tufaidi maana hii nchi sio ya baba yenu bali ni yetu sote.[emoji57]
Usijifariji mkui.
Watu wa Pwani mnaendekeza starehe sana bila kuwekeza.
Hakuna mkoa ambao serikali iliwajaza wananchi pesa mfukoni wala kuwajengea nyumba.

Mnaendekeza ki..t..omba..na sana na maneno mengii mnasahau kupambana msomeshe watoto.

Nchi hii ni kaskazini, Kanda ya Ziwa kiasi na nyanda juu kusini hasa Iringa na Mbeya ndio wananchi wanapambana kujiendeleza na kusomesha watoto na leo hii elimu imeleta matunda katika mikoa hiyo.
Acheni uvivu japo sio wote.
 
Back
Top Bottom