TANZIA Rubani wa Ndege iliyotekwa 1982 kushinikiza Nyerere ajiuzulu afariki dunia

TANZIA Rubani wa Ndege iliyotekwa 1982 kushinikiza Nyerere ajiuzulu afariki dunia

RIP kapteni Mazula.
Kuna yule jamaa mfupi hivi alikua Capten atcl ndio alimrudisha baba wa taifa( RIP)toka huko matibabuni ng'ambo akiwa kafariki(madai yake)
Sijui yupo hai yule ama.
Jina lake nimesahau
 
View attachment 2076364

Rubani wa Ndege iliyotekwa mwaka 1982 na vijana waliokuwa wakishinikiza Mwalimu Nyerere ajiuzulu, amefariki dunia.

Capt Deo Mazula alifariki tarehe 6 Januari 2022 na Kesho (Januari 11, 2022) anatarajiwa kuzikiwa jijini Arusha katika Makaburi ya Njiro.

Unaweza kusoma kuhusu kisa cha kutekwa kwa ndege hii, hapa Nini kilipelekea vijana wa Tanzania kuteka ndege ya ATC 1982 Mwanza?
Asante kwa taarifa hii, tulikuwa tunakaa nae mtaa mmoja Drive In Flats, na mdogo wake pia alikuwa Pilot wa ATC.

Rip Capt. Mazula.
P
 
Hivi Kuna Ndugu Mwingine Aliitwa George Mazula?? Naye alikuwa Rubani ATC?? Naomba Kufahamishwa Tafadhali
Walikuwa ni mtu na kaka yake, na wote brand cars zao zilikuwa ni Volvo, enzi hiyo mawaziri gari zao zikiwa ni Pegeot 504 number zikiwa STC na STD!. Gari za polisi zilikuwa Landrover 109, na escort ya Nyerere ilikuwa Peogeot 404. Benzi yenyewe ya Nyerere naomba nisiseme, ila kulikuwa na mhindi tajiri kwa jina la Lord Rajipar, akaleta Benz kali kuliko ya Rais, S Class 500 miaka hiyo!. alitiwa ndani kwa uhujumu!.
Rip Capt. Mazula umetukumbusha mbali!.
P
 
Watu humu kumbe ni wakongwe.
Sisi wenye 30's tunawasikiliza nyie tu
Humu kuna member nilimsaidiaga kufungua akaunti alizaliwa mwaka 1948. Vijana wakimtukanaga yeye huwa anatukana kwa mdomo mi huwa nacheka sana.
Sema mzee mwenyewe ni mjanja mjanja halafu mcheza bao na draft kidogo kwa hiyo ana yale matusi ya utani utani.
 
He was very-cool huwezi kumdhania. Baadae alisoma sheria na amepractise kwa muda alikuwa na ofisi pale new red cross miaka ya 2014, RIP.
Boss wangu wa zamani, na zungu lake,very calm na usingeweza amini kama ni mtu wa matukio
 
Hivi Kuna Ndugu Mwingine Aliitwa George Mazula?? Naye alikuwa Rubani ATC?? Naomba Kufahamishwa Tafadhali
Yupo George alikuwa anasoma Tambaza. Hawa nadhani walikuwa brothers wawili wote marubani.
George pia amefarika zamani kabla ya 2009. George ndiye mtoto wake aliuawa Marekani katika ugomvi wa kugombania demu.
 
Walilikuwa ni mtu na kaka yake, na wote brand cars zao zilikuwa ni Volvo, enzi hiyo mawaziri gari zao zikiwa ni Pegeot 504 number zikiwa STC na STD!. Gari za polisi zilikuwa Landrover 109, na escort ya Nyerere ilikuwa Peogeot 404. Benzi yenyewe ya Nyerere naomba nisiseme, ila kulikuwa na mhindi tajiri kwa jina la Lord Rajipar, akaleta Benz kali kuliko ya Rais, S Class 500 miaka hiyo!. alitiwa ndani kwa uhujumu!.
Rip Capt. Mazula umetukumbusha mbali!.
P
Mkuu Paskal, kuna mambo ya zamani ukiyakumbuka unabaki kufurah…enzi za “nenda kwa singasinga ndo utapata spare hii” huwa sisahau huu msemo maarufu wa mzee wangu hapo akinutuma kununua spare ya Bedford au Zepha 6!
 
Walikuwa ni mtu na kaka yake, na wote brand cars zao zilikuwa ni Volvo, enzi hiyo mawaziri gari zao zikiwa ni Pegeot 504 number zikiwa STC na STD!. Gari za polisi zilikuwa Landrover 109, na escort ya Nyerere ilikuwa Peogeot 404. Benzi yenyewe ya Nyerere naomba nisiseme, ila kulikuwa na mhindi tajiri kwa jina la Lord Rajipar, akaleta Benz kali kuliko ya Rais, S Class 500 miaka hiyo!. alitiwa ndani kwa uhujumu!.
Rip Capt. Mazula umetukumbusha mbali!.
P
Duu umenikumbusha benzi ya mzee Aikaeli Mbowe ikaja imeandikwa jina kila kifaa
 
Back
Top Bottom