Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,455
- 73,145
Nimekukubali wewe ni wa wakati wetu. Umenikumbusha vituko vya Profesa Shaba hasa akisha piga vitu vyake. Mmoja ya wataalamu mahiri wa sekta ya afya kupata kutokea kwa wakati uleMiaka yake ya mwisho akiwa hai alikuwa akishinda pale maeneo ya Pegeout karibu na ilipokuwa bushtrekker. Alikuwa mtu poa sana, akiniona lazima anisalimie.
Walikuwa members wa Gymkhana Club miaka ile, ndio wajanja wa mjini enzi za Nyerere anaondoka anaingia Mwinyi,
Alikuwepo mtu mmoja akifanya kazi habari Maelezo akiitwa Abdallah Ngororo, kila nikifuata bia za wazee Chinese au IFM usiku ninamkuta anapata kinywaji akiwa na hayati Jaji Mapigano, Profesa Shaba na wazee wengine wa mitaa ile.