Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Akitokea THT ni binti mnyange aliyetikisa anga la muziki wa bongo fleva mwaka uliopita..
Ana kipaji
Ana mvuto
Ana sauti
Lakini akakosa miongozo sahihi...utoto na pengine ulimbukeni wa kuwa maarufu ghafla kutokana na tungo zake tamu vilimchanganya hata kufikia kujiona kuwa sikio lake ni kubwa kuliko kichwa
Taratibu akaanza dharau na nyodo, akawadharau hata wadau muhimu kwenye industry, akatema bazoka kwa njugu za kuonjeshwa
Sasa Ruby wa mwaka jana si wa mwaka huu! Si habari tena, wengi wamepotea kwa njia hii list ni ndefu sana na hii yote imetokana na kujikweza na kulewa sifa haraka sana kabla ya mafanikio