Rufaa dhidi ya African Lyon: Yanga kupewa alama zake 3 walizocheza dhidi ya African Lyon?

Acheni figisufigisu chezeni mpira mnyama mbele kwa mbel[emoji12] [emoji12]
Figisu zipi hizo?

Mbona hampendi sisi tufanye figisu ili hali nyinyi mlifanya figisu za Kessy mpaka mkapata elfu 50'000/= zenu.

Au ndio mmegoma kabisa kufanya Fair Play kwenye tasnia ya soka Kama mlivyogoma Dhidi ya JKT Ruvu? [emoji23]
 
Kwa wenzetu mata nyingi utasikia kupigwa faini timu au wachezaji na hata marefa lakini wanajitahidi sana kuwa matokeo ya uwanjani yasiguswe na mtu!
Kwa hivyo unamaanisha hata kama kanuni haisemi A basi Kamati inamue kusema B kwakuwa bila hivyo Kamati itaonekana inapendelea mtu fulani!!!!!?

Si ndio!!!?
 
Yanga imeshawahi kukatwa points 3 mechi na Coastal union sababu ilimchezesha canavaro akiwa na kadi tatu za njano.. Wakatwe tu
Wao wanataka kuona Kanuni za ligi zikiwanufaisha wao tu.

Ila inapoonekana kanuni zinainufaisha Klabu ya Mabingwa watetezi wa "LigiKuu Tanzania bara".... unaanza kuona wivu wa kike. [emoji23]
 
Unajua kusoma kweli isije kuwa nabishana na mental case.Aliyekata rufaa ni Ndanda. Naona hujui hata una comment nini.
Uwezi ukaelewa, ili hali una Mahaba na upande wako!

Ukiona umepungua mahaba unaweza kurudi upya ukasoma.

Nina imani utaelewa tu.
 
Kumbuka KESSY AMEANZA KUCHEZA HUKU MKATABA UKIWA UMEISHA.
 
Yanga walipe kwanza 50,000,000/= za Simba Kama ni pointi inabidi nayo Yanga ikatwe pointi zote alizocheza Kessy kabla hajakamilisha taratibu za kuhamia Yanga.
Ni aibu timu Kama Yanga kulilia point za mezani baada ya kushindwa kupambana uwanjani.
Kessy kacheza mechi nyingi bila kukamilisha taratibu za uhamisho,, hata hizo nazo zikatwe tu.
 
Tatizo paka hawajui kanuni ndiyo maana kelele haziishi


HUWA WANAJIFANYA TO ANAJUA SANA KANUNI....

ILA UKIFIKIRIA SANA UNAKUTA HATA KANUNI ZA KIMIKATABA YA BAADHI YA WACHEZAJI WAO WANASHINDWA KUZIELEWA...


NDIO MAANA KWA MIAKA MINGI WAMEKUWA WAKIKIMBIWA NA WACHEZAJI KWA MAKOSA YA KIMIKATABA.
 
Tuongee tu ukwel wa mungu ni kwamba ukiona timu imeanza kulalamika lalamika na kuanza kuomba point za mezani bas ujue mambo yako tight.

Cmba safar hii ni ubingwa tu labda dunia ipasuke.
Kipindi unalalamika Yanga SC ipokonywe alama zote alizomchezesha Kessy.... Haikuwa kulalamika na kutaka Ubingwa wa mezani bila kupata ushindani?
 
Tusubiri maamuzi ya kamati husika.

Sheria na kanuni vichukue mkondo wake.

Mwisho was msimu kila team itakaa kwenye nafasi yake stahiki! Stahiki!
Naam!

Nafasi yao stahiki. Nimekuelewa.
 
Ni vizuri kupata ufafanuzi pale taratibu zinapokiukwa,lakini haitasaidia lolote ikiwa utaratibu huo unaongozwa na mhemuko wakuongeza points. Tuache matokeo ya uwanjani yaamue na sio mezani.
Basi kanuni zinazotoa point za mezani zifutwe. Acha kuongea kwa mhemko, zungumza kikanuni. Soka linaongozwa na kanuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…