Rufaa dhidi ya African Lyon: Yanga kupewa alama zake 3 walizocheza dhidi ya African Lyon?

Ngoja nisaidie kumuelezea:-

Kessy kasajiliwa kipindi "Mabingwa watetezi na wa kihistoria wa LigiKuu Tanzania bara" wakiwa kwenye michuano ua kimataifa kwa lengo la kutumika kule.

Kipindi anasajiliwa alikuwa eligible kucheza ligi na Caf. (kwa mujibu wa mkataba mpya).

Ila ameanza kucheza/kutumikia Klabu kipindi ambacho Mkataba wake umeisha! Hivyo mechi yeyote aliyo cheza katika kipindi hiko haiwezi kuathiriwa kwakuwa anakuwa amecheza akiwa nje ya muda wa mkataba wake wa zamani.

Kosa ambalo limepigiwa faini ya Mil 50 ni lile la kumsajili akiwa bado na mkataba na Klabu yake ya zamani na klabu yake ya zamani haijafikiana naye muafaka wa kuvunja mkataba ili ajiunge na Klabu nyingine yeyote.

sasa hapa kama hujaelewa! duh.
 
Mkuuu.....
Umejaaliwa maelezo mengi yaliyojaa ushabiki....unashindwa kuelewa hoja ya msingi kwa kessy.....

Labda tu nikukumbushe kuwa lalamiko la wana Simba ni kuwa Yanga wamemtumia kessy hali ya kuwa sio mchezaji wao na bado alikuwa na mkataba na Simba......shauri ambalo Simba wameshinda baada kamati kuona kuwa Yanga wamekiuka taratibu....na kamati ikaamuru kuwa vijana jangwani wailipe Simba milioni hamsini....

Sasa swali linasemaje......

Kama kamati teure imegundua uharamia waliokuwa wakitaka kuufanya Yanga na kuwapiga faini.......

Je zile mechi walizomtumia kessy hali ya kuwa sio mchezaji wao......kwa mujibu wa hukumu ya kamati zina uhalali gani......!??
 
Ikiwa mkataba wake uliiisha....kosa la Yanga ni lipi hadi kutakiwa kuilipa Simba milioni hamsini.....!!??
alianza kutumikia yanga kabla ya tarehe15june ambapo mkataba WA simba na kessy uliisha,hapo namaanisha kuvaa jez,kwenda kambi na hasa yanga kutuma jina la kess June 10.akuwa na mkataba na simba wakati ligi inaanza.nathani Imeeleweka mkuu
 
Kwa hiyo hukumu inayoitaka Yanga kuilipa Simba milioni hamsini ni kwa ajili ya kuvaa jezi za Yanga....na kuhudhuria mazoezi ya Yanga....???
 
Imeiadhibu au imejivua lawama......sasa kama wameona kessy hakuwa na uhalali Yanga....na kutozwa milioni...hamsini.....hizo mechi alizocheza kessy Yanga zina uhalali gani.....!!??
Tatizo la Kessy na la huyu ni mawili tofauti, Kessy hakucheza ndani ya mkataba bali alionekana kwenye mazoezi na kwenda Uturuki, ndiyo maana Simba ikidai fidia na siyo point maana hakucheza mechi yoyote, sasa huyu amecheza na amefunga wakati hajamaliza taratibu za usajiri kutoka Mbao Fc.
 
ushabiki unakusumbua sio bure,mkataba WA kess na simba uliexpire june15 2016,kuwa mnasoma hukumu hizo makini,ndo maana kessy Hana hatia wala nn,
 
Ukizungumzia mafanikio vyura fc watasubiri sana kwa mnyama bro we kausha tu endelea kugoogle
Mafanikio gani unayoyazungumzia wewe?

1.
Mapinduzi Cup?
Tusker?

2.
Au kucheza fainali enzi zile za caf?

Kama ni namba 1 basi unahaki ya kujivunia hayo mafanikio. Maana mafanikio ya tournaments ndogondogo kama hizo haziongezi credits kwenye rank za CAF Zzinazoonyesha orodha ya Klabu bora zaidi.

Kama ni namba 2 mafanikio. Basi tuseme sasa hayo ndio mafanikio yanayoendana na hadhi ya Klabu yako... Maana hata FC Simba (Inashiriki Uganda Premier League) ishawahi kushiriki Caf Final mwaka 1972......hivyo basi hatu pasa tuseme ndio klabu yenye mafanikio kuliko SC Villa (Uganda).
 
Tff wajinga sana
Sasa walipitishaje jina LA jamaa wakat usajiri wake bado una matatizo?
 
Simba ndio mabingwa wa kihistoria wa Cecafa champions.
 
Ahh ulikuwa hujaanza kupenda mpira. Google na hiyo.
 
Simba ndio mabingwa wa kihistoria wa Cecafa champions.
Kwa klabu inayojitambua haiwezi umiza vichwa kwenye tournaments ndogondogo kama hizi.

Hazina credits kwenye viwango vya CAF RANKS
 
Wacha uvivu Google umeanza kupenda mpira mwaka jana?
 
Jibu la swali lako utalipata kwa kuangalia Mkataba wa Kessy na Simba unaisha Tar Ngapi...?

Na mechi Kessy amwanza kucheza tar Ngapi...?

Ukipata Jawabu la hilo swali na ukalinganisha aina ya Kesi iliyofunguliwa na Uongozi wa simba dhidi ya suala la Kessy utagundua kitu.
 
Hizi point za mezani sio nzuri tuna wachezaji wakulipwa basi tuwatumie/watumike kwa %100 kuiletea timu ushindi fikiri kama tungeshinda tuwaaminishe wachezaji wetu kuwa hakunaga ushindi mwingine nje ya dakika 90 ili ushinde itakubidi uwe na nidhamu ya mchezo uwezo wa kushinda stamina/pumzi ubora wa kikosi chako
 
Venance Ludovick amesimamishwa kucheza VPL mpaka suala lake litakapokamilika kusikilizwa, mpaka sasa imebainika ni kweli ana leseni mbili zilizotolewa na TFF ambazo ni za kuchezea Mbao na African lyon, kwenye usajili wa mtandao TMS jina la Ludovick kule Mbao linasomeka Ludovick lakini African Lyon linasomeka Ludovic huku herufi K ikiwa imeondolewa, imeagizwa katika kikao kijacho wote kwa maana ya Mbao Fc ,African Lyon pamoja na mchezaji wafike na vielelezo vyao vyote ili wafikie tamati, suala la African Lyon kupokwa point halitakuwepo kwa kua mpaka mchezaji anacheza tayali alipewa leseni na mmlaka halali TFF hivyo kosa linakua kwa TFF kumpa mtu leseni bila ya kikao cha kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kukaa means atakayeadhibiwa ni officer wa TFF aliyetoa leseni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…