Rufaa dhidi ya African Lyon: Yanga kupewa alama zake 3 walizocheza dhidi ya African Lyon?

Rufaa dhidi ya African Lyon: Yanga kupewa alama zake 3 walizocheza dhidi ya African Lyon?

Mkuu unajisumbua bure....

Hawawezi kupokwa point hata moja bali wao ndio watakao ongezewa point hata kama ni za uzushi....kwa kuwa TFF ndio wameshaamua Yanga....awe bingwa ligi wa miaka yote....

Ndio maana haishangazi kukuta katika mechi ya Yanga mwamuzi anafungiwa kwa maamuzi mabovu.....huku waao wakiendelea kupeta....
Sasa Mkuu umeona wapi Duniani adhabu kwa kosa la Muamuzi linaathiri matokeo ya Uwanjani.....


Hivi kwa mfano kwenye mechi ile, baada ya Tambwe kufunga lile bao na muamuzi kuita kati. Mlitarajia TFF wafute matokeayya mchezo wa ligi kweli?


Sasa kama huo ndio utaratibu.... Inamaana kila mechi ya LigiKuu Tanzania bara itakuwa inarudiwa kwa sababu waamuzi wamekosea kuzichezesha. Kwa sababu hakuna mechi ya Ligi kuu inaisha bila Muamuzi kukosea.

Sasa kila mtu akigaka mechi yake irudiwe kweli itakuwa Ligi au Kituko..... (Kwa sababu vpl ndio Itakuwa ligi ya kwanza Ulimwenguni kuwa na kanuni ya namna hiyo).

Tuache unafiki kwanza, then tucheze mpira.
 
kwa kungwi kukiliwa na kwa somo kuliwe
Kumbe mnajua. Ilanajitiaga ukichaa tu.

Mlitaka alama za Yanga SC ziliwe kupitia Kessy, ila hamtaki Yanga SC ile kupitia kwingine.... [emoji23]

Sheria ni msumeno! Lazima ikate pale panapostahili.
Na sio pale uonapo panastahili.
 
Ngoja na mnyama naye auwashe moto wa Kessy kisha tuone wao watapokwa point ngapi.
 
Kumbe mnajua. Ilanajitiaga ukichaa tu.

Mlitaka alama za Yanga SC ziliwe kupitia Kessy, ila hamtaki Yanga SC ile kupitia kwingine.... [emoji23]

Sheria ni msumeno! Lazima ikate pale panapostahili.
Na sio pale uonapo panastahili.
Venance Ludovick amesimamishwa kucheza VPL mpaka suala lake litakapokamilika kusikilizwa, mpaka sasa imebainika ni kweli ana leseni mbili zilizotolewa na TFF ambazo ni za kuchezea Mbao na African lyon, kwenye usajili wa mtandao TMS jina la Ludovick kule Mbao linasomeka Ludovick lakini African Lyon linasomeka Ludovic huku herufi K ikiwa imeondolewa, imeagizwa katika kikao kijacho wote kwa maana ya Mbao Fc ,African Lyon pamoja na mchezaji wafike na vielelezo vyao vyote ili wafikie tamati, suala la African Lyon kupokwa point halitakuwepo kwa kua mpaka mchezaji anacheza tayali alipewa leseni na mmlaka halali TFF hivyo kosa linakua kwa TFF kumpa mtu leseni bila ya kikao cha kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kukaa means atakayeadhibiwa ni officer wa TFF aliyetoa leseni
 
Ngoja na mnyama naye auwashe moto wa Kessy kisha tuone wao watapokwa point ngapi.
Suala la Madai yenu halina "Mashiko" ndio maana lina hang hang tu sasa hivi.

Hata viongozi wenu hawajui la kufanya.

Kila kitu kimestack kuhusu hiyo kesi henu. Mmefikia wapi kuelekea FIFA?
 
Suala la Madai yenu halina "Mashiko" ndio maana lina hang hang tu sasa hivi.

Hata viongozi wenu hawajui la kufanya.

Kila kitu kimestack kuhusu hiyo kesi henu. Mmefikia wapi kuelekea FIFA?
Fifa? Sasa hivi wanadai ml 50 wapunguze madeni ya tra
 
Tatizo ni mchezaji kuchezeshwa au mchezaji kuwafunga ndala fc?
Mchezaji yeyote wa Kitanzania kuifunga Yanga SC, it's like a dream come true!

Ndio maana Kichula alipofunga bao kwenye Derby alimwaga Machoni mithili ya mvua ya mawe.

Hiyo yote ni furaha.

Inatokana na ukubwa na jina la Klabu. Nikuulize wewe sasa hivi.... Hivi utajisiliaje ukipata nafasi ya kufunga dhidi ya Real Madrid...? Utajisikia sawa na kupata nafasi ya kuifungia timu yako bao dhidi ya Queen's Park Ranger FC?

Jibu kaa nalo.!
 
Hizi point za mezani sio nzuri tuna wachezaji wakulipwa basi tuwatumie/watumike kwa %100 kuiletea timu ushindi fikiri kama tungeshinda tuwaaminishe wachezaji wetu kuwa hakunaga ushindi mwingine nje ya dakika 90 ili ushinde itakubidi uwe na nidhamu ya mchezo uwezo wa kushinda stamina/pumzi ubora wa kikosi chako
Hatuja sema tunataka alama za bure ili tuchukue Ubingwa.

Ubingwa ni lazima hata bila alama hizo.
 
Naam naona kama kuna "mabingwa" wa kihistoria hebu nielewesheni huo ubingwa unapatikanaje?
Ni rahisi sana Mkuu!

Bingwa hupatikana kila baada ya ukamilisho wa mechi takriban 30 za vilabu 16.

Yule aliye maliza akiwa angani ndiye hutawazwa bingwa.

Hapo kwenye neno 'Mabingwa' huenda nikawa nimekosea... si unajua lugha yetu hij ya kiswahili..

Wachache sana wanayoiweza, (kama nyinyi) ila sisi wengine ni watumiaji tu.
 
Ndani ya saa 24 yatatoka Majibu ya Rufaa iliyokatwa na Mabingwa wa kihistoria wa LigiKuu Tanzania bara yaani Dar es Salaam Young Africans SC.

Kamati hiyo ndiyo yenyejukumu la kuamua kama Yanga inastahili alama mbili au kuendelea kuwa nyuma kwa alama nne kama ilivyokuwa sasa.
Klabu ya Yanga SC inaweza kupunguza gepu la alama 2 kati yake na wale waliowashikia nafasi yao, endapo tu itashinda rufaa yake iliyoikatia timu ya African Lyon, kwa kumchezesha mchezaji Venance Ludovic, huku akiwa hajakamilisha taratibu zake za uhamisho kutoka Mbao FC ya Mwanza.

Meneja wa Yanga Hafidhi, Salehe ameviambia vyombo vya habari, baada ya kupata taaarifa sahihi kuhusiana na mchezaji huyo waliamua kuwasilisha malalamiko yao kwa kamati ya rufaa iliyochini ya TFF, ili haki iweze kutendeka kama ambavyo sheria zinavyosema.

“Tulipata maelekezo ya kutosha na mchezaji huyo aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Awadhi Juma, na ndiyo alifunga bao la Lyon kabla ya sisi kusawazisha mchezaji huyo hajakamilisha taratibu zake za usajili kutoka Mbao na hata Mbao wenye wamemkatia rufaa,”amesema Hafidhi Afisa wa Yanga SC.

YANGA inaweza kukomboa pointi mbili ilizopoteza kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya African Lyon baada ya sare ya 1-1 Desemba 23, mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kamati ya Saa 72, ambayo ndiyo inayosimamia ligi ya Vodacom inakutana leo na moja ya kesi ambazo itazisikiliza na kuzitolea maamuzi ni hiyo ya Yanga dhidi ya Lyon, kuhusiana na kumchezesha mchezaji huyo.

Lyon inadaiwa kukiuka taratibu za kumsajili mchezaji huyo kutoka timu ya Mwanza na rufaa mbili zimegongana mezani, moja ya Yanga na nyingine ya Mbao.

Klabu zote mbili Mbao na Yanga zinapinga Ludivic kuichezea Lyon akiwa mchezaji halali ya Mbao aliyoichezea mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Vodacom Tanzania.

Kwa mujibu wa vielelezo vilivyowasilishwa na Mbao, inaonekana kabisa Ludovic alihamia Mbao kimakosa na akatumika kimakosa pia, hivyo Yanga inaweza kushinda rufaa hiyo na kuvuna pointi mbili zaidi.

Katika mchezo huo uliopigwa Desemba 23, kwenye uwanja wa Uhuru, timu hizi zilimaliza dakika 90, zikitoka sare kwa kufungana bao 1-1, na kupoteza malengo ya Yanga katika kuwafukuzia wapinzani wao Simba ambao walikuwa wanapishana kwa pointi mbili.

Endapo Yanga itashinda rufaa hiyo basi itafikisha pointi 42 na kupunguza gepu la pointi kati yao na Simba kutoka nne hadi mbili kama ilivyokuwa awali.
c69c4496bc50d5e4111d6912e5538140.jpg

-nawasilisha
Hiyo kamati isisahau na magoli ya mkono ya yanga dhidi ya timu zingine.
 
Sasa Mkuu umeona wapi Duniani adhabu kwa kosa la Muamuzi linaathiri matokeo ya Uwanjani.....


Hivi kwa mfano kwenye mechi ile, baada ya Tambwe kufunga lile bao na muamuzi kuita kati. Mlitarajia TFF wafute matokeayya mchezo wa ligi kweli?


Sasa kama huo ndio utaratibu.... Inamaana kila mechi ya LigiKuu Tanzania bara itakuwa inarudiwa kwa sababu waamuzi wamekosea kuzichezesha. Kwa sababu hakuna mechi ya Ligi kuu inaisha bila Muamuzi kukosea.

Sasa kila mtu akigaka mechi yake irudiwe kweli itakuwa Ligi au Kituko..... (Kwa sababu vpl ndio Itakuwa ligi ya kwanza Ulimwenguni kuwa na kanuni ya namna hiyo).

Tuache unafiki kwanza, then tucheze mpira.

Hata lile goli Lao tata kipa kasukumwa na mshambuliaji wa Simba eti wanaamini refa aliona kipa anapoteza muda
 
Vepeee kikao cha mezani cha point 3 ...nasikia majibu tayari...[emoji23][emoji23]
 
Tuongee tu ukwel wa mungu ni kwamba ukiona timu imeanza kulalamika lalamika na kuanza kuomba point za mezani bas ujue mambo yako tight.

Cmba safar hii ni ubingwa tu labda dunia ipasuke.
Baelezee baelezeee
maamuz ya kamat.yashatoka na hakuna cha point 3 wala three points [emoji23][emoji23]
 
Alama zisingekuwa za muhimu, hakuna mtu angesumbuka kukata rufaa!

Kwenye mchezo wa soka alama 3 ni muhimu sana. Ukuona mpinzani amefanya makosa yanayokinzana na Kanuni lazima aadhibiwe!

Inakuwaje kila mtu angekuwa anatafuta alama 3 nje ya kanuni.? Kungekuwa na mpira kweli?

Au kwa sababu ni Yanga SC, basi wapotezee kwakuwa alama 3 kwao hazina umuhimu?

Taratibu zifuatwe!
Waliokaa nafasi za watu wanaanza kuhara sasa. [emoji23]
Mchezo uwanjani mezani nini,siyo siasa hiyo
 
Back
Top Bottom