Rufaa ya kina Mdee mbele ya Baraza Kuu dhidi ya Kamati Kuu CHADEMA: Kicheko kwa G19, Kilio kwa kina Mbowe

Rufaa ya kina Mdee mbele ya Baraza Kuu dhidi ya Kamati Kuu CHADEMA: Kicheko kwa G19, Kilio kwa kina Mbowe

Yaani hawa mkiwasamehe tutadili nao mitaani, watakula Sana manati
Na mtafungwa sana tena sana..acheni kutumia au kujidai mnajazba.

Yaani hata wale waliohukumiwa kunyongwa kwa mauaji ya Alphonce Mawazo hawajawapa funzo?
 
View attachment 1662261
Mhe Halima Mdee na wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai, baada ya kula kiapo hivi karibuni.

Sasa ni wazi kwamba, Mheshimiwa Halima Mdee na wabunge wenzake 19, ambao ni viti maalum kupitia Chadema, watarudishiwa uanachama wao asubuhi na mapema siku Baraza Kuu la Chadema litakapokutana kusikiliza rufaa yao waliyoiwasilisha kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chadema, juzi tarahe 27 Desemba 2020.

Akiongea na mtandao wa Mama Amon, Mbunge mmoja wa viti maalum, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kwamba, kwa mujibu wa barua ya tuhuma dhidi yao, Mdee na wenzake 18 wanakabiliwa na mashitaka sita. Anayataja hatua kwa hatua kama ifuatavyo:

“Mosi, tunatuhumiwa kupora madaraka ya Kamati Kuu ya Chama kwa kushiriki katika mchakato wa kula njama ya kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kuwa kinyume cha ibara ya 7.7.16(q) inayotamka kwamba kazi za Kamati Kuu zitakuwa ni pamoja na kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge, na Baraza la Wawakilishi.”

“Pili, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kupanga njama za kuhujumu chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka kanuni ya 3(a)(i) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”

“Tatu, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kupinga misimamo ya chama hadharani na nje ya vikao vya chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(a)(iii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”

“Nne, tunatuhumiwa kufanya kosa la kujihusisha na matumizi mabaya ya madaraka/upendeleo kwa kujipatia huduma au manufaa binafsi kinyume na taratibu kwa kutumia vyeo vyetu, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(e)(ii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”

“Tano, tunatuhumiwa kufanya kosa la kukiuka sharti linalotamka kuwa kila kiongozi anatarajiwa awe na msimamo wa kuaminika, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.2(iv) ya Kanuni za Chama.”

“Na sita, tunatuhumiwa kufanya kosa la kukiuka sharti linalotamka kuwa kila mwanachama anatakiwa kujiepusha na upinzani dhidi ya chama na wagombea wake na makundi ya majungu ya kugonganisha viongozi na wanachama hasa wakati wa chaguzi, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.3(iv) ya Kanuni za Chama.”


View attachment 1662269
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akiwa anapanga mikakati ya kisiasa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema

Baada ya kuzitaja tuhuma zao zote, Mbunge huyo anaongeza kusema kuwa, “tayari tumejibu tuhuma hizo na majibu yetu hayana chenga hata kidogo.”

Mbunge huyo alifafanua kuwa majibu yao yako katika makundi mawili. Katika kundi la kwanza, watuhumiwa wanakanusha tuhuma zote kama zilivyoorisheshwa hapo juu. Anasema kuwa, barua za tuhuma zilikuwa na ukurasa mmoja usio na ufafanuzi wowote unaowawezesha kufanya utetezi wenye mashiko.

Na katika sababu zilizo kwenye kundi la pili watuhumiwa wanahoji uhalali wa mchakato ulioutumika kuwatia hatiani.

“Mosi, katika suala la maudhui ya tuhuma, kwa kuwa uteuzi wa wabunge hufanywa kutokana na ushirikiano kati ya Ofisi ya Katibu Mkuu na Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na sisi sio sehemu ya ofisi yoyote kati ya ofisi hizo mbili, ni wazi kwamba sisi hatukujiteua, na hivyo, anayepaswa kuulizwa nani alifanya uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum wa Chadema ni ama Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, au Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Mahera, au wote wawili, lakini sio vinginevyo,” anasema Mbunge huyo.

“Na unajua baadhi yetu tulikuwa mikoani siku zile za uteuzi, kwa maana kwamba hatukuwa Dar es Salaam wala Dodoma. Ni kwa vipi tumepewa tuhuma eti za kula njama na kujiteua?” anauliza Mbunge huyo.

“Pili, ni kuhusu utaratibu. Kwa kuwa, kabla ya kikao baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, kama vile Matibu Mkuu, John Mnyika, walikuwa mstari wa mbele kutumia mainstream and social media (vyombo vya habari vya kimapokeo na mtandao ya kijamii) kutushambulia wakijitapa kwamba wanasubiri kula vichwa vyetu, ilikuwa ni wazi kwamba, hata ndani ya kikao hakukuwa na utulivu wala usalama unaoweza kuruhusu hoja zikatolewa, kusikilizwa na kuamuliwa kwa haki bila jazba na mapigano. Ni kama tulikuwa tayari tumehukumiwa,” anasisitiza Mbunge huyo.

“Na tatu, ni kuhusu utaratibu pia. Kwa mujibu wa kanuni za natural justice (kanuni za haki asilia) tulifukuzwa bila kusikilizwa. Lakini, sio haki kumhukumu mtu ambaye hujamsikiliza. Tuliomba tuhakikishiwe usalama lakini hawakutuhakikishia usalama wowote. Kulikuwa na waandamanaji Makao Makuu ya Chama na kule kwenye barabara inayokwenda hotelini ambako kikao kilipaswa kufanyika. Hata kama kulikuwa na dharula, Kanuni ya 6.5(d) ya chama inasema kuwa mtuhumiwa lazima apewe haki ya kusikilizwa, ama kupitia mkutano wa uso kwa uso au mkutano wa kidijitali inaoruhusiwa na Kanuni za chama,” alifafanua Mbunge huyo.

Sasa unasubiriwa utaratibu wa kichama kuitisha Baraza Kuuu ili kusikiliza na kuamua rufaa hizi kumi na tisa.

Takribani, mwezi mmoja uliopita, Kamati Kuu ya Chadema ilifikia uamuzi huo wa kuwavua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa mujibu wa ibara ya 5.4.4 ya Katiba ya Chama baada ya kuridhika kwamba walikiuka Katiba, Kanuni na Maadili ya Chama.

Aidha, Kamati Kuu iliwavua nyadhifa zote walizokuwa nazo ndani ya Chama na hivyo kuwataka kukabidhi mali za Chama walizokuwa nazo, sambamba na kuwazuia kujihusisha na masuala yoyote yanayokihusu Chama.

Kwa mujibu wa nakala za barua za tuhuma zilizo mikononi mwa mtandao wa Mama Amon, watuhumiwa wote walipewa njia mbili za kupitia. Njia ya kwanza ni kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.3 na 6.5.8 ya Kanuni za Chama.

Na njia ya pili waliyopewa watuhumiwa, kama mbadala, ni kuandika barua ya kuomba kurejea kwenye chama kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.4 ya Kanuni za Chama. Watuhumiwa wote waliamua kupitia njia ya kwanza, yaani njia ya kukata rufaa.

Kwa sababu ya uamuzi wao huu, jana mtandao wa
mwanahalisioniline.com, unaomilikiwa na kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, inayoongozwa na Saed Kubenea, uliwashutumu wabunge hawa ukidai kwamba, "kina mdee wameanzisha vita mpya Chadema," kwa sababu ya uamuzi wao wa kukata rufaa badala ya kuandika barua ya kuomba uanachama.

View attachment 1662268

Sehemu ya ukurasa kwenye gazeti la Saed Kubenea, liitwalo Mwanahalisionline.com, ukwatuhumu kina Mdee kuanzisha vita ndani ya Chadema

Hata hivyo, Mbunge aliyeongea na mtandao wa Mama Amon amepinga mtazamo huo. “Kwa kuwa haki ya kukata rufaa ipo kikatiba, sioni kwa nini vyombo vya habari vya kina Kubenea vinakuwa na mtazamo hasi dhidi ya uamuzi wetu,” alionyesha mshangao.
Huu ugoro umekuingizia sh ngapi ewe kibwengu????
 
Mkuu mama Amon ni mmoja wa Covid-19, hilo wala usiumize kichwa chako.
Huyu Mama Amon Typically ni mmojawapo wa COVID-19. CHADEMA ipo kwa sababu ya umoja na masikilizano na kufuata taratibu za viongozi wake ndio maana ikawepo na ikiwa na mshikamano kamili mpaka hivi leo just image kikawepo chama ambacho kila mmoja anafuata taratibu zake ni niini kinaweza kutokea au je kunaweza kuwapo kwa chama hapo.
 
Wewe uliona wapi jumuiya ya wanawake inaongozwa na " msichana"?

Chadema wanavuna walichopanda!
Wacha dharau wewe yule bimkubwa kabisa unasemaje ni msichana? Hata ustaadh Rashid alimlinganisha na Bikidude, yule amejaaliwa baby-face tu lakini amekula chumvi ya kutosha.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Hii hoja ya kuwepo waandamanaji ni dhaifu na watashindwa akina Mdee hata waende wapi.

Ni maandamano gani ambayo Polisi imeshindwa kuyazuia hapa nchini.

Polisi huzuia hata vikao vya ndani sembuse hayo maandamano.

Kulikuwa na waandamanaji Makao Makuu ya Chama na kule kwenye barabara inayokwenda hotelini ambako kikao kilipaswa kufanyika
 
Napendekeza wakati chama kinakamilisha kuwafutilia mbali hawa waliojiteua, kipendekeze na kupeleka majina mengine rasmi kwa idadi hiyo ili kutendea haki nafasi hiyo ya viti maalum
 
Hizo hoja umeziandika kiushabiki sana, hayo majibu unayoyaita ya "uhakika" kwangu sijaona uhakika wowote, hao wanawake walikosea usije kuwatetea hapa kwa kigezo cha "haki za wanawake"

Lazima sheria na taratibu zifuatwe siku zote regardless ya jinsia ya mtu.
 
Back
Top Bottom