Rufaa ya mchezaji Langa Lesse Bercy wa Congo Brazzaville

Rufaa ya mchezaji Langa Lesse Bercy wa Congo Brazzaville

Mambo ya tz bwana utacheka sana
Yaaani kulia lia tu tu
Kama ile ya alikiba hahahahahahahaha
Afu tunajitaidi kudai haki wakati huku watu wamenyimwa ajira na wanadaiwa mkopo lakini hii hatuidai
serikali imeajiri chini ya watu laki 5,watz wapo 50m,kama unafikiri tatizo la taifa ni mikopo ya elimu na ajira serikalini,fikra hzo mnazo wachache,pana mengi ya kufanya
 
Tanzania nchi ilivo na gundu hatuwezi kushinda hiyo rufaa hata iweje
 
Hii kitu CAF hawatoa jibu?

Kama jamaa aliitwa na TFF wameingia gharama, inakuwaje?

Huyo kijeba si rahisi kwenda kujisalimisha CAf hadi waseme wataiondoa Congo kama haendi kufanya kipimo.
 
Tunataka tupitie mlango wa nyuma? TFF nashauri waachane tu na hii habari, tutaenda kutia aibu huko.
Mamelodi Sundowns wametwaa Champions League ya Africa unajua kuwa walishatolewa na wale waCongo!? Fair play ni pamoja na kuheshimu vigezo na masharti ya mchezo.
 
Mamelodi Sundowns wametwaa Champions League ya Africa unajua kuwa walishatolewa na wale waCongo!? Fair play ni pamoja na kuheshimu vigezo na masharti ya mchezo.
bila masharti,sheria inakuwa siyo game
 
Hao CAF hawana akaunti ya instagram tukawanyooshe kwa matusi?
 
Hii inshu iliishia wapi asee au ndo muendelezo wa upumbavu wetu watanzania
 
Malinzi yuko kwenye kampeni. Wengine pale TiFitiFu hawana habari.
 
Kwa nini TFF haitoi taarifa kwa wananchi kilichojili, wao huwa wanaomba tu ushirikiano siku za mechi maana kuna mahesabu.
 
Kwa nini TFF haitoi taarifa kwa wananchi kilichojili, wao huwa wanaomba tu ushirikiano siku za mechi maana kuna mahesabu.
Kinachokera zaidi hata waandishi wa habari hawahoji chochote kuhusu hilo
 
Kinachokera zaidi hata waandishi wa habari hawahoji chochote kuhusu hilo
Siku wakijua wahoji na gharama tulizotumia ktk hii rufaa mbuzi ,usikute ili njia ya kupiga hela tu,wajumbe walioenda ni wangapi na akina nani?
 
Kama ilivyoripotiwa hapo awali, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya kutoridhika na kujiridhisha kuwa mmoja wa wachezaji wa Jamhuri ya Congo-Brazzaville, alikiuka kanuni za mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, mwaka huu lilimkatia rufaa mchezaji Langa-Lesse Bercy katika Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).

Kutokana na rufaa hiyo dhidi ya mchezaji huyo wa Congo, Langa Lesse Bercy, CAF liliagiza apelekwe Makao Makuu ya Shirikisho hilo, lililoko Cairo, Misri kwa ajili ya kurudia na kuthibitisha umri wake kwa kipimo cha MRI (Magnetic Imaging Resonance).

TFF iliagizwa na CAF igharimie zoezi zima ikiwa ni pamoja na kulipia gharama za usafiri wa mchezaji husika na daktari wake pamoja na kulipia gharama za vipimo. TFF ilikubaliana na matakwa hayo ya CAF na kulipia.

Kipimo ilikuwa kifanyike leo Novemba 19, 2016 saa 5.00 asubuhi mjini Cairo, Misri. Ujumbe wa TFF wa watu wanne ukiambatana na madaktari wawili uliwasili mjini Cairo tangu Novemba 17, 2016 ili kuwa shuhuda wa zoezi la kipimo hicho.

Jana usiku saa 5.00 TFF ilipokea ujumbe kutoka CAF kuwa mchezaji Langa Bercy ameshindwa kusafiri kwenda Cairo kwa kuwa yuko katika eneo lililoko "vitani",eneo hilo halikutajwa.

TFF inaendelea kufuatia kwa karibu jambo hili ili kuhakikisha haki inatendeka .

Kadhalika Aidha TFF inaomba wadau wa mpira wa miguu wawe na subira katika kipindi hiki.
Hahaha ..changa la macho...hapo watu walitaka hy hela waitoe wafanye kampeni...
 
CAF YAWAPA CONGO MUDA WA MWISHO KUMTUMA LANGA BERCY KWA AJILI YA VIPIMO,WAMETOA SIKU KUMI KUANZIA JANA WAWE TIYARI WASHAMTUMA.
 
Back
Top Bottom