chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Mbombo ngafu, haijaisha mpaka iishe, kama haitoshi kwa mafuriko yanayotokea sasa Rufiji, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetangaza uwepo wa mvua kubwa katika maeneo kadhaa, pamoja na Mkoa wa Pwani.
Tahadhari za awali ni pamoja na kuwaondoa wakazi wa mabondeni, misaada iwe standby Rufiji, na pia wakazi wa mabondeni wizara ya ardhi ichukue hatua ya kuwapimia viwanja uwanda wa juu, Jerry Silaa aache kuhangaika na vipisi vya migogoro, awe waziri wa kitaifa.
Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa ipige kambi Rufiji.
Pamoja na Wizara ya Afya, kwa kuwa magonjwa mlipuko ni nje nje, maliasili wakaangalie jinsi ya kuongoza tembo na mamba zao zisiumize wananchi.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kitaifa, wananchi wanataka waone uhalali wa wewe kukalia kiti hicho, maana mpaka sasa uwepo wa jeshi lako haujaonekana Rufiji, wananchi wanaokoana wao kwa wao. Huna kikosi maalum cha uokoaji kinachoweza kwenda haraka? Mbona Magereza wana "FFU", Jeshi lina Millitary Police (MP), na Polisi wana FFU? Haya, chukua kikosi chako maalum, chenye mafunzo maalum, tia timu Fufiji umheshimishe Mama Samia
Wale wataalamu walio-study tabia ya mto rufiji wakae na serikali watengeneze Environmental Impact Assessment ili udhibiti wa mto Rufiji iwe component ya mradi wa bwawa la Julius Nyerere