Rufiji Kumenoga: TAZARA yanunua behewa la tani 200 kubebea mitambo bwawa la Mwalimu Nyerere isiyobebeka kwa barabara

Rufiji Kumenoga: TAZARA yanunua behewa la tani 200 kubebea mitambo bwawa la Mwalimu Nyerere isiyobebeka kwa barabara

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
TAZARA imesema imenunua behewa lenye uwezo wa kubeba tani 200 litakalotumika kubeba mizigo ya bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere iliyozidi uzito au upana wake unazidi kiwango cha upana unaopaswa kusafirishwa kwa barabara.

Msemaji wa TAZARA amesema behewa hilo limenunuliwa kwa dola za kimarekani milioni moja na litatumika kubeba mitambo kama mota za kuzalishia umeme(Turbine) kutoka Dar mpaka stesheni ya Fuga.

Tangu mradi wa Mwalimu Nyerere umeanza, TAZARA imeshabeba tani 700,000 kwenda Fuga.

Zaidi, Jisomee HAPA

200-Ton Well Wagon loaded with concrete blocks for testing.JPG
 
Yaani kitu kilichoonekana ni upigaji tu hakuna zuri lililoonekana katika hii habari. Haya mnaojua bei halali ya hilo behewa tuambieni ili nasi tuunge mkono kuwa tumepigwa.
 
Kama viieite zinanunuliwa kama njugu, wacha tuambulie hata hili behewa la kusaidia kazi muhimu.
 
Maaneeneerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr kama huo mchuma bilioni basi mie bongo sirudi asilani
 
Kwani kwanini mmeamua kubisha hiyo bei?

Nyie mnajua yanauzwa bei gani hayo ma lowloader wagons?
 
Back
Top Bottom