beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Shule nne za msingi zilizopo katika kata ya Muhoro, wilayani Rufi ji, mkoa wa Pwani zimefugwa baada ya kuzingirwa na maji ya mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.
Shule zilizofungwa ni hizo Nyambapu, Muhoro, Kingongo na Kipoka na jumla ya wanafunzi ambao wameathirika na hali hiyo hivyo kukosa kosa masomo ni 3,435.
Mbali na shule hizo, pia hekta za mazao 4,000 na kaya 3,600 zimeathirika na mafuriko hayo. Kutokana na shule na baadhi ya shule kuathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini na wanafunzi na walimu kushindwa kufika madarasani, Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, amewataka wakuu wa wilaya nchini kuwatafutia shule mbadala wanafunzi ambao shule zao zimefungwa kutokana na mafuriko zikiwemo hizo nne za mkoa wa Pwani.
Jafo alitoa agizo hilo mjini Kibaha juzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kikao cha ushauri cha mkoa mkoa huo (RCC). Alisema mwaka huu kumekuwa na mvua nyingi, hali ambayo imesababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo na shule kuzingirwa, hivyo kushindwa kuingilika na baadhi ya wananchi kuhama kwenye makazi yao.
“Nawaagiza wakuu wa wilaya nchini kuangalia njia mbadala ya kuwasaidia wanafunzi hasa wale wanaotarajia kufanya mitihani ya taifa ili waendelee kusoma wakati serikali inaangalia namna ya kufanya,” alisema.
Jafo ambaye ni Mbunge wa Kisarawe, mkoani Pwani, alisema mvua zimeleta madhara makubwa na kuharibu miundombinu ikiwamo barabara na miundombinu mingine.
“Madhara ya mvua ni makubwa sana, hivyo tuna wajibu kama viongozi kuweka mazingira ya kuwaondolea adha wananchi kipindi hiki kigumu cha mvua,” alisema Jafo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, alisema wilaya ya Rufiji ndiyo imepata madhara makubwa ya mvua hizo na kusababisha athari za mafuriko. Alisema baadhi ya kaya zimehamia kwa majirani ili kupata hifadhi ya muda baada ya nyumba zao kukumbwa na mafuriko na maeneo mengine hayaingiliki kutokana na maji kujaa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo, alisema wilaya hiyo imeathiriwa kwa kiasi kikubwa hasa vijiji vilivyopo jirani na mto Rufiji na kusababisha shule katika maeneo hayo kufungwa.
Alisema kijiji cha Muhoro kimeathirika kwa kuzungukwa na maji na kusababisha nyumba na biashara kufungwa kutokana na maeneo hayo kujaa maji.
Chanzo: Habari Leo