Ruge achemsha: Fiesta yamdodea

Ruge achemsha: Fiesta yamdodea

inawezekana huyo Alaine ni msanii mkubwa lakini sio maarufu hapa bongo. mwenye nyimbo zake atuuploadie na sie tusiomfahamu tumsikie.

Anaimba sweet reggae pamoja na akina Romain Virgo, Berres Hammond, Tyrus,etc ingia u tube
 
Angeletwa Romain Virgo mngeona, hawa jamaaa majuu wana rock sana
 
tetetete jamaaa mleta uzi nourmaa kweliiiii....
 
Alaine ni mkali wa riddim asikwambie mtu, fanya kama una download ngoma yake hii hapa: mp3skull.com/mp3/alaine_another_love_song.html

All in all, kikubwa nafikiri Clouds walikua wanatumia mpunga mrefu kuwaleta wasanii wa marekani na kuwalipa mkwanja mrefu ila wabongo nao ambao wanaperform kwenye fiesta pia wameshtuka wanataka nao wapewe mpunga wa kueleweka hivyo kuminimize cost ikabidi clouds wasake wasanii wasio na gharama kivile.
 
Ikiwa imebaki siku chache kufanyika tamasha kongwe la Fiesta,kumetokea kuzorota na kukosa msisimko kabisa kwa tamasha ili tofauti na miaka ya nyuma..ni kana kwamba Ruge mwaka huu ategemee maumivu makali sana kwa uchache wa maudhurio.

Hali hii sijui imetokana na nini,ni kukosa jipya(ubunifu)? wananchi kukinai? au tukio la Eatv kuwa pre empty kwa kutangaza vizuri show ya Psquaire.?

Labda kukosekana kwa msanii wa kimataifa wa kueleweka,maana wasanii toka nje wa safari hii ni utumbo mtupu sijui Davido,Jmartins, Allein yani ni bora wangemaimamisha Diamond kuwa main perfomer,pengine hii nayo imechangia.

Ila kwa kifupi Ruge na fiesta mwaka huu wamefulia mpaka noma sanaa!!

Tunasubiria Show ya Psquaire.

huyu jamaa jina lake kamili ni rugemalila mutahaba au?
 
Kwanza wote wanafik tu,Mie nianze kwa kutoa shavu kwa mtoa uzi,kweli tamasha la kimama sana hili,mimi siendi hata ctaki kusikia,Alaine kweli n mkali anahit song kama "your me na amepewa shavu kwa Wyre wa kenya "nakupenda pia" sema nn hapo bdo hawajamfikia dogo DOMO hata nusu,hii imewadodea P square ndo mpango.R.I.P Fiesta
 
Hapa kila mtu anaongea kwa mapenzi yake binafsi. Ukweli unabaki palepale Alaine ni msanii mkubwa na huwezii ukamweka level sawa na Domo na Nature. Hata mm Nature na Domo nawakubali sana, Swala la kushangiliwa jukwaani sio inshu. Kwa sisi mashabiki wa Riddim Alaine tunampa Respect kubwa. Alafu tambueni Tanzania kimziki tupo nyuma. Hata siku wakiletwa Morgan Heritage wataonekana wa kawaida 7bu watu wengi sio wafuatiliaji wa Ridimms mbalimbali. Hivyo kosa la Clouds ni kuleta msanii ambaye mziki anaofanya haushabikiwi sana nchini Tanzania.

MORGAN HERITAGE habari nyingine hiyo. Hata 70,000/= kiingilio naingia.
 
10/10...na huwezi mshindanisha Alaine Laughton na Domo au Nature kwenye jukwaa la Fiesta Bongo...tuwatupe O2 Arena London, wote sio kwao, halafu tuone nani atamkalisha mwenzie. Ni sawa na kuhoji kama Domo au Nature wanaweza mkalisha Alaine kwenye jukwaa ndani ya Kingston Jamaica.

Morgan Heritage ni hadithi nyingine baba...angalia concert zao walizofanya Ulaya (UK, Sweden, Belgium, Finland etc..) ni balaa, huwa wanajaza viwanja vya mipira wale! Ni moja kati ya wanamuziki ambao concert zao ni ghali..

Nafatilizia concert zao nyingi. Wajamaa ni noma,halafu kilakitu live. Sidhani hao watakaokuja katamasha ka fiesta watakuja na band?
 
Mkuu Pantheraleo hawa Royal Family ni balaa.
Nikikumbuka Live in Amsterdam daah

listen good,
The best Rasta known created from the Jamaican land,
but we love to fly over to Amsterdam,
Huyo ndio Peetah morgan.
 
ukweli ndo huo,hyo fiesta ishabuma mapema japo bdo event yenyewe haijafanyika.Kwa kuangalia tu,u can see the very big difference ya mwitikio wa mashabiki tofauti na fiesta zilizopita.Sio mpaka msubirie outcomes after event ndo mpate cha kuongea,mengine yanaonekana wazi wazi.
Mnaoenda,safari njema hiyo kesho!!!
 
huyu jamaa jina lake kamili ni rugemalila mutahaba au?

Ndio uyo,,na kama nilivyowaambia awali show ilikuwa mbaya kupitiliza......wasanii wameshindwa kuimba....sound mbovu kupindukia.....wasanii wa kimataifa wameiponda sana maandalizi mabovu..........bangi imevutwa waziwazi kuanzia backstage hadi kwa mashabiki.........ikafikia hatua hadi umeme ukazima kwenye steji....kila mtu alitoka amenuna kuanzia wasanii mpaka mashabiki.....umati nao ulikuwa mdogo sana kulinganisha na show za nyuma.....watu walikuwa wanashangilia msanii akiitwa stejini akianza kuimba wanapiga kelele shukaaaaaa!!jinsi walivyoboa(no reharsal japo kuna bajeti ya hii kitu toka kwa mdhamini).Mimi sikuenda na ninazidi kujipongeza kwa nini sikuenda kwenye izo fujo za jana...Kifupi Fiesta ya jana imejizika yenyewe.
 
ukweli ndo huo,hyo fiesta ishabuma mapema japo bdo event yenyewe haijafanyika.Kwa kuangalia tu,u can see the very big difference ya mwitikio wa mashabiki tofauti na fiesta zilizopita.Sio mpaka msubirie outcomes after event ndo mpate cha kuongea,mengine yanaonekana wazi wazi.
Mnaoenda,safari njema hiyo kesho!!!


Ilikuwa ni aibu,,wasanii wa nje wameondoka wakitucheka.

Tusubirie ya P Squaire
 
Yaani huna tofauti mwanamke muuza papuchi

Mkuu nasikia Ruge kaomba msamaha kwa aibu iliyotokea jana...na katangaza wasanii watarudia tamasha kwa kiingilio cha bure leo hii juma2????Uyu mtu ana laana za watu wengi sana ndio maana siku izi mikosi haimuishi.
 
Back
Top Bottom