Imethibitika umefariki kaka!
Ni dhahiri pasi Na shaka kwamba sehemu yenye utajiri Mkubwa kuliko zote hapa duniani ni makaburini; Fikra , mawazo Na ndoto bora zenye kuutajirisha ulimwengu zimezikwa!
Kwa Mara ya kwanza nimeonana nawe Mwaka 2013 nikiwa EATV wakati ambao nilisimamishwa kazi baada ya kuweka maudhui Fulani mtandaoni, ulitaka niwe sehemu ya vijana wako wa clouds 360, katika mazungumzo tukagundua wote tuna upenzi wa kusoma vitabu..uliniita bwana mikakati.
Duniani kuna watu wa tabia tofauti, kuna wapenda vitu, fedha nk..ukikutana na Ruge hakuwa akikupa fedha Bali maarifa, amesaidia Na kujenga vijana wengi hasa Kwa maarifa ya kimaisha..mara ya mwisho tulionana mahali tukazungumza Kwa SAA 3, sikuwahi kujua kama unakijana wa rika langu..ulinijuza Na Kwa Bahati nilikutana nae mahali Fulani kikazi.
Thamani ya Ruge Kwa wengi ni zaidi ya kipande cha ardhi cha Nyamongo chenye dhahabu inayofikia wakia milioni 36!
Ruge ulikua ni zaidi ya utajiri wa gesi yenye ujazo wa futi tril.26.99 ambayo ni sawa Na Mapipa bil.4.86!
Ulikua kaka, baba Na boss Kwa wengi!
Hakika makaburi yameelemewa Na utajiri!
Pumzika Kwa amani Mzee wa mikakati..tutakukumbuka daima!
Adrian!