Kama mnavyojua Ruge Mutahaba ni mtoto wa Profesa Mutahaba wa Bukoba Vijijini, Tarafa ya Kiamutwara, Kata Karabagaine ,Kijiji Kabale, Kitongoji Kiziru -Muzira mbogo, Muhabarishaji yuko huko anatutumia updates moja kwa moja tunaweka hapa
Kwa wanaokaa maeneo ya Bukoba,
Eelekeo wa mazishi yatakapofanyika nyumbani kwao Mutahaba kama watokea mjini, Ni Barabara ya kibeta kama waelekea Muleba, ukifika Magoti Km 3 kutoka Bukoba mjini utakutana na Kibao cha Gereza Rwamulumba, unapita Itahwa, Karabagaine ndo unafika kabale/kiziru kwa mzee Mutahaba, ni km 8 kutoka bukoba mjini,
Wadau mbali mbali wa maeneo yanayopakana na mazishi yatakapofanyika wameshaanza kukusanyika wakitokea
Nsisha, Kangabushro, Itahwa, Magoti,Kitwe, Katoma,Itahwa na Rwamulumba ,
Maoni ya watu waliowengi wanasema kwamba ni kweli jamaa alikuwa maarufu ila hawakujua kama ni wa maeneo hayo, kwasababu ukilinganisha jina lake na maendeleo ya eneo lile ni kama vile hakutenda haki, japokuwa wanasahau kwamba Ruge alikuwa ni mtu wa masuala ya burudani tu na mtu mmoja hawei kuleta maendeleo ya wilaya nzima isipokuwa wa kulaumiwa kama kuna ishu ya kulaumu ni Mzee Mutahaba mwenyewe na maprofesa wanaomzunguka,
Kwa haraha haraka pale kuna maprofesa si chini ya wanne, kuna mabalozi waliowahi kuwa mabalozi na walioko ubalozini kama mabalozi sasa si chini ya watano,
Kuna watu wengi sana ambao kwa pamoja wangeweza kushirikiana kuleta kinachostahili,
kwa Bahati mbaya aliyesema hivyo ni kwa mshtuko wa kuona kumbe mtoto wa Mutahaba ni maarufu vile lakin kwa haraka haraka maendeleo wanayo japokuwa binadamu huwa hawaridhiki na kuna slogan imeshajengeka kwamba wahaya wanajenga kwingine siyo kwao,,
SALAAMU ZA RAMBI RAMBI TOKA KWA MKUU WA MKOA WA KAGERA KWENDA KWA FAMILIA YA MUTAHABA
Maandalizi ya Nyumba ya Milele ya Marehemu Ruge Mutahaba
TAIFA LIMEPOTEZA MOJAWAPO YA VIJANA WAPAMBANAJI
UPDATES
HABARI: Msemaji wa familia ya Mutahaba, Kashasha amesema Rais John Magufuli ametoa ndege kwa ajili ya kusafirisha mwili wa Ruge Mutahaba na waombolezaji siku ya Jumapili kwenda Bukoba atapozikwa-MCL
MKUU WA MKOA AWASILI MSIBANI NA KUKUTANA NA KAMATI YA MSIBA
Hapo Ni Mmiliki wa Shule ya Josiah Grils Bwana Ruga Masabala akisalimiana na Afande alifika Msibani
Mwonekano wa Juu wa Nyumbani kijijini kwa Ruge Mutahaba