TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

We nae hebu fatisha uliponiquote uone nilichokimaanisha

Kwenye msiba wa Ruge siku ya kumuaga pale bukoba mjini katika viwanja vya gymkhana mc walikuwa ni Hassan Ngoma na Babie Kabae

Kama ni kuhusu bambataa la kitinda mimba alivaa mkoti mkubwa na bado wambea tuliliona lishape
Tumeelewana nadhani
Ya kibonde???

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Screenshot_2019-03-13-16-48-53-1.png
 
We nae hebu fatisha uliponiquote uone nilichokimaanisha

Kwenye msiba wa Ruge siku ya kumuaga pale bukoba mjini katika viwanja vya gymkhana mc walikuwa ni Hassan Ngoma na Babie Kabae

Kama ni kuhusu bambataa la kitinda mimba alivaa mkoti mkubwa na bado wambea tuliliona lishape
Tumeelewana nadhani

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chritiana Mutahaba ambaye ni mama mzazi wa marehemu Ruge Mutahaba amesema familia yake itafarijika iwapo mazuri aliyoanzisha mwanaye yataendelezwa kwa kuwa inaonekana aligusa maisha ya wengi.
Akizungumza leo Machi 6, 2019 katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na televisheni ya Clouds, amesema amesikia mengi kuhusu mwanaye ambayo hakuyafahamu lakini itakuwa faraja yake yakiendelezwa.
“Mpaka sasa najiuliza huyu Ruge ni nani, amewafanya nini Watanzania, mbona amepata heshima kubwa, mbona mdogo sana lakini amezikwa kwa heshima hivi. Lakini nitafutahi kuona ndoto zake zinaelezwa,” amesema.
Amesema ukiacha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, mwanaye amekuwa Mtanzania wa pili kupata heshima kubwa katika mazishi yake.
“Wakati Mwalimu Nyerere anafariki hatukuwepo nchini lakini tulifuatilia mazishi yake yalikuwa makubwa sana, tangu hapo sijaona tena, kwa kweli amepewa heshima kubwa ninashukuru,” amesema katika mahojiano yaliyofanyika katika Kijiji cha Kiziru, Bukoba.
Pia, amemshukuru Rais John Magufuli na viongozi wengine walioshiriki kufanikisha maziko ya mwanaye kwa hali na mali.
“Namshukuru Mungu aliyetuwezesha kuleta mwili wa Ruge mpaka Bukoba, nawashukuru viongozi wa Serikali kuanzia Rais John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Kagera na wote waliotusaidia. Pia, nawashukuru Watanzania kwa maombi yao.”
Akinukuu vitabu vya dini amesema mkono wa mwanadamu ni mfupi kwamba kuna mahali unaishia na ndivyo ilivyokuwa kwa Watanzania walioshiriki kwa hali na mali kuokoa uhai wa Ruge wakati akiugua.

" Tunashukuru kwamba Ruge ametuachia Watoto asingetuachia tungeumia zaidi " - Mama Ruge
 
Back
Top Bottom