Rugemalila aitaka Benki Kuu iwataje watu wote waliopata mgawo wa Escrow. Gavana asita, aomba ruhusa ya Mahakama awataje

Hivi fedha zilizowekwa kwenye magunia na magunia kuwekwa kwenye malori zilielekea wapi?
 
Lakini hii awamu chini ya Jemedari JPM imejimbanaua kupapambana na ufisadi, inakuaje tena bado kuna watu wanalindwa?!
Kama Kuna mtu anaamini ufisadi unapingwa kwa maneno Mungu amsaidie tu
 
Kwani ile orodha ilifia wapi au haijawahusisha waliopata mgao kwenye sandarusi, hii nchi imewahi kupata majizi aisee.....
 
Kwanini mkuu?

In God we Trust
Haiwezekani Gavana wa BOT apate kigugumizi cha kuwataja waliopata mgawo wa Escrow ili hali wanajulikana na wananchi tunawajua halafu pale Yupo mahakani kwa hiyo kuwataja sio kosa na wala hakuwaingizi hatiani. Je, GAVANA HAJUI WALIOHUSIKA AMA NI UHUNI INA MAANA AMESHINDWA KUMTAJA HATA NGELEJA NA PROF ANNA NTIBAIJUKA...WALIOPEWA MKIMGAO KIDOGO...
 
Hivi wakionekana hawana hatia watapewa fidia?
Tangu mwanzo wa kukamatwa, binafsi sijaona hatia. Unawezaje kujidai kuwa unashughulikia ufisadi wa escrow kwa kumuweka kikwete nje? Drama Magufuli.
 
Kama ni professor Tibaijuka, huyo alipewa na Rugemarila kupitia mkombozi Bank. Governor hawezi kutaja JK et- al. Na hapo ndo kwenye kiini.
 
Nawewe mmbeya umeona hiyo ndiyo news ya kuyolea povu, badala ya kuandika juu ya mafanikio makubwa yanayofanywa na Serikali, umeendekeza udaku, uchochezi, unafiki, ujinga na upumbavu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani wewe ndo unatoa povu.Nakushangaa swala la maendeleo ya serikali na mgao wa escro umelioainishaje,na kutajwa kwa wahusika wa escro au na wewe ulipata mgao ndo maana unafoka.Yeye anaitaka benki kuu iwataje ndo hoja yake hapo.Kama hujui au huelewi kilichozungumzwa achia nafasi kaa kimya.
 
Rugemalira simuombei mabaya zaidi ya hayo yaliyomkuta ila naota umauti ukimkuta kabla kesi yake haijamalizika.
P
 
Chonde chonde wasije wakammalizia huko gerezani
Kwa sababu hana cha kupoteza tena ni bora angetaja hayo majina hata akimaliza safari yake duniani either kwa matakwa ya Mungu ama binadamu basi ukweli uwe umejulikana.
Sent using Jamii Forums mobile app
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…