Rugemalila aitaka Benki Kuu iwataje watu wote waliopata mgawo wa Escrow. Gavana asita, aomba ruhusa ya Mahakama awataje

Rugemalila aitaka Benki Kuu iwataje watu wote waliopata mgawo wa Escrow. Gavana asita, aomba ruhusa ya Mahakama awataje

Ruge anatapa tapa
Angejikita katika kupangua kesi yake,ingeweza kumsaidia zaidi kuliko kujaribu ku 'crowd the deck' ili wafe wengi
 
Majizi na mafisadi ya CCM yatamuua huyu mzee kabla hajatoka gerezani. Ni bora awataje tu yeye mwenyewe.

Huyu amefanywa kafara, hii ni aibu ya mwaka - badala ya kufatilia wahujumu walio gawana fedha za Escrow na kuzibeba kwenye mifuko ya Rambo, badala yake wanamkalia kooni NSHOMILE wa watu ili wapoteze lengo la kuwakamata the brains behind the scum.

Ruge kajieleza vizuri kwamba yeye aliuza shares zake na kulipwa na PAP, hakuchukua hata senti tano za ESCROW sasa kwa nini Dola linamkalia kooni kwa story za kutunga tu - si tunajinadi kimataifa kwamba Taifa letu ni transparent, sasa mbona linaonekana ni translucent linapata kigugumizi kuwataja waporaji wa fedha za ESCROW.

Looking back now nakumbuka vizuri kauli ya Mweshimiwa fulani aliye wahi kusema fedha za ESCROW hazina mwenyewe in other words zilikuwa zina float tu awaiting kikundi cha watu wajanja wachache to grab them at opportune time - don't expect the list will include average "Kalubandika".

Cha muhimu hapa ni kumuomba our Maker ili Regu atoke Gerezani akiwa safe and sound.
 
Mstaafu alipiga na yeye? Ntacheka sana akitajwa[emoji23][emoji23][emoji2357]

Sent using Jamii Forums mobile app
Kunakipindi kama nilisikia anasema hizopesa sio zetu sasa sijui kwanini zinaendelea kudaiwa.
Ngoja tuone awamuhii ya kutetea rasilimali za wanyonge itakuwaje.

In other hand kunasauti anasema wastaafu waachwe wapumzike.

Shkamoo siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walisha kula kiapo kulindana hao, sasa tumuombee mzee Rugemalila ili awataje ingawa itamuweka pahali pasipo salama sana
Haiwezekani Gavana wa BOT apate kigugumizi cha kuwataja waliopata mgawo wa Escrow ili hali wanajulikana na wananchi tunawajua halafu pale Yupo mahakani kwa hiyo kuwataja sio kosa..na wala hakuwaingizi hatiani....Je GAVANA HAJUI WALIOHUSIKA AMA NI UHUNI INA MAANA AMESHINDWA KUMTAJA HATA NGELEJA NA PROF ANNA NTIBAIJUKA...WALIOPEWA MKIMGAO KIDOGO...

In God we Trust
 
Ruge anatapa tapa
Angejikita katika kupangua kesi yake,ingeweza kumsaidia zaidi kuliko kujaribu ku 'crowd the deck' ili wafe wengi

How do you mean!! Your comments sounds a bit strange - don't you think?
 
Mnasihi,
Unadhani kati ya BoT na Ruge nani ataaminika zaidi akitaja hayo majina?Mkuu Ruge anaakili si kilaza kama wewe.Katika nchi yenye vilaza wengi, Ruge akitaja majina wanasiasa wa ccm kwa kuwa wanajua ukilaza wenu watakuja na hoja nyepesi tu mfano.

Ruge alikuwa amepandwa na maleria kichwani alipokuwa anataja majina yale na wanaweza wakamtafuta daktari njaa ili aje kudhibitisha uongo wao,mwisho wa siku vilaza wote mnaamini kuwa yale majina hayakuwa.

ya kweli ila malaria ilimpanda mtu kichwani na mchezo unaishia hapo
 
Mtemi Chenge hajarudisha na tena anasema hakuna wa kumgusa!

Mtemi huyu kuna kitu anaji amini, hata ukimwangalia body language yake ana ujasiri husio wa kawaida!! Watu watasema maneno chungu mzima mengi yakiwa ni ya kubuni tu lakini uki-check Mtemi wa watu anaonekana yuko as cool as cucumber.

Sasa wakifanya makosa ya kumfuata fuata nina hakika atafumua a Pandora box, sioni kama wahusika wanaweza kufanya such grave mistake.
 
Yeye awataje tu,tuwajue na mwaka wa uchaguzi huu ndio mzuri

Sent using Jamii Forums mobile app

Mimi nina wasi wasi kwamba hata Ruge akiwataja Mahakamani sioni kama vyombo vya habari vitakuwa na ujasuri wa kuchapicha majina kwenye magazeti yao aukwenye online TV,

vile vile Hakimu anaweza kutupilia mbali ushauri wa Ruge wa kutaka kutaja majina ya watu walio gawana fedha za ESCROW - kesi nzima inaonekana ni political dynamite - kumbuka huu ni mwaka wa uchaguzi naona watakubali yaishe kimya kimya without offending anyone - my opinion.
 
Back
Top Bottom