Rukwa: Adaiwa kumuua mkewe kwa kumnyonga akimtuhumu kuchepuka, naye ajiua kwa kujinyonga

Rukwa: Adaiwa kumuua mkewe kwa kumnyonga akimtuhumu kuchepuka, naye ajiua kwa kujinyonga

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi.JPG

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Tanga, iliyopo Mkoani Tanga, Emmanuel Jerome (32), anadaiwa kumnyonga mke wake, Lucy Nshoma (34), katika nyumba ya kulala wageni mkoani Rukwa, kisha na yeye kujinyonga kwa kutumia kamba juu ya mti siku moja baadaye Mkoani Katavi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Ali Makame amesema marehemu ni mkazi wa Tanga na chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi.

Kamanda Makame amesema marehemu Jerome alikuwa na mgogoro na mke wake, ambapo alimtuhumu kutoka kimapenzi na wanaume wengine.

Alisema Jerome na mkewe walipanga safari kuelekea mkoani Rukwa, ambapo ni nyumbani kwao marehemu mke wake na walifikia nyumba ya kulala wageni Julai 26, 2022, ndipo usiku alipochukua uamuzi wa kumnyonga mkewe.

Kamanda Makame alisema baada ya kumnyonga katika nyumba hiyo ya wageni, aliacha ujumbe wa maandishi kwa ndugu wa mke wake ambao ni mashemeji zake uliosomeka: "Nisameheni kwa yaliotokea".

Alieleza kuwa baada ya kufanya tukio hilo mkoani Rukwa alikimbilia mkoani Katavi na Julai 27,2022, huko mtaa wa Ilembo, Manispaa ya Mpanda, alichukua uamuzi wa kujinyonga na walikuta mwili wake ukiwa unaning’inia kwenye kamba.
 
Huyu ticha nae sijui kafanya nini sasa ila hakuna shida tayari ndio ashajipiga kamba
 
Ukiachilia mbali stress za nyongeza ya mshahara maisha magumu nk . Kuna haja ya serikali kutahadharisha watu juu ya hasira za waalimu huku mitaani, juzi ticha mmoja kapasua chupa muhudumu wa bar kisa chenji 2000.
 
Lazima watu tujifunze ku control hasira za papo hapo. Huyu itakuwa hasira zilifanya aue na baadae guilty ikamshambulia na majuto ndio maana akaona ajiue na yeye.

Ukiwa na hasira ni bora uondoke uende mbali kwanza au upate mtu wa kumsimulia kwanza.
 
Dah, Pole sana Mwalimu na marehemu wote. Tusipende sana kuchukulia mambo ya duniani haya too serious. Kuna wakati tujifunze kuwa easy taker.
 
Wananishangaza sana hawa wanaoua bila tahafhari yoyote.

Hawaangalii hata movie wala kusoma vitabu kupata ABC za kukwepa vyombo vya dola na kupoteza ushahidi.

Bahati mbaya kuua sio kazi yao, wenye kazi zao huwa sio issue sana kuukwepa mkono wa dola. Hawa wengi wakishatoa roho majuto huanza na mjukuu huzaliwa.
 
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Tanga, iliyopo Mkoani Tanga, Emmanuel Jerome (32), anadaiwa kumnyonga mke wake, Lucy Nshoma (34), katika nyumba ya kulala wageni mkoani Rukwa,

Hivi umesoma hichi juu ulichokiandika [emoji115]

Mnaandika habari haraka haraka mnakimbizwa na nini
 
utelezi tena😅😅katobo kanapeleka watu kasi sana dah...wapumzike kwa amani
Acha kabisa mnasilaha moja matata ya maangamizi.
Tena kama wewe unaonekana kabisa mtu akipata utelezi wako it will certainly be an unforgettable experience😝 no pun intended🤣🤣🤣🤣
 
Acha kabisa mnasilaha moja matata ya maangamizi.
Tena kama wewe unaonekana kabisa mtu akipata utelezi wako it will certainly be an unforgettable experience😝 no pun intended🤣🤣🤣🤣
😅😅😅wacha nishushie comment yako kwa pepsi baridi.....
 
Back
Top Bottom