Rukwa: Adaiwa kumuua mkewe kwa kumnyonga akimtuhumu kuchepuka, naye ajiua kwa kujinyonga

Rukwa: Adaiwa kumuua mkewe kwa kumnyonga akimtuhumu kuchepuka, naye ajiua kwa kujinyonga

Lakini vyovyote vile hakustahili kuuwawa.

Bora angemuacha tu maana kumuacha mtu nako ni adhabu kubwa sana na ya kutosha tu.

Halafu kusikiliza upande mmoja na kufanya hukumu naona kama si Sawa.

Pengine naye angepewa nafasi ya kujieleza labda angeweza kueleweka na jamii.
Upande wa pili pia tumeusikia maana jamaa kaweka viambata vya mwanamke anavyo panga ratiba za kwenda kuuchezea kwingine

Wala haitaji kumsikiliza mwanamke maana amewakilishwa na audio zake
 
Ni muda umefika wizara ya elimu ianzishe Somo la Saikolojia kuanzia shule za msingi. Hapo mambo ya ushauri nasaha na unasihi yatafundishwa kwa undani na watu wengi watapata elimu ya kujitambua uwezo na udhaifu wao na hivyo kuweza kujichukua wenyewe (self) bila kutoa madhara kwao na kwa wengine.
 
Lucy mapenzi Kwa jamaa yalishakwisha alikuwa akitafuta sababu Tu
 
View attachment 2307819
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Tanga, iliyopo Mkoani Tanga, Emmanuel Jerome (32), anadaiwa kumnyonga mke wake, Lucy Nshoma (34), katika nyumba ya kulala wageni mkoani Rukwa, kisha na yeye kujinyonga kwa kutumia kamba juu ya mti siku moja baadaye Mkoani Katavi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Ali Makame amesema marehemu ni mkazi wa Tanga na chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi.

Kamanda Makame amesema marehemu Jerome alikuwa na mgogoro na mke wake, ambapo alimtuhumu kutoka kimapenzi na wanaume wengine.

Alisema Jerome na mkewe walipanga safari kuelekea mkoani Rukwa, ambapo ni nyumbani kwao marehemu mke wake na walifikia nyumba ya kulala wageni Julai 26, 2022, ndipo usiku alipochukua uamuzi wa kumnyonga mkewe.

Kamanda Makame alisema baada ya kumnyonga katika nyumba hiyo ya wageni, aliacha ujumbe wa maandishi kwa ndugu wa mke wake ambao ni mashemeji zake uliosomeka: "Nisameheni kwa yaliotokea".

Alieleza kuwa baada ya kufanya tukio hilo mkoani Rukwa alikimbilia mkoani Katavi na Julai 27,2022, huko mtaa wa Ilembo, Manispaa ya Mpanda, alichukua uamuzi wa kujinyonga na walikuta mwili wake ukiwa unaning’inia kwenye kamba.
Mwanaume yeyote ambaye akili yake inateswa na mapenzi hana akili, mwanaume yeyote anayeteswa na mwanamke kwasababu ya wivu wa mapenzi ni chizi. ukishindwa kuwa na kiasi kwenye hii dunia utaumia kupita kiasi..
 
Neskiliza hizi voice notes, kwakweli mwamba alikua mwamme mvumilivu
Mapenzi ya upande mmoja, na kutokuwa na kipato.

Kwa nilivyozisikiliza Lucy hakuwa na mapenzi na Emma, Emma alikuwa analazimisha mapenzi na mbaya zaidi Lucy amemfanyia Emma vituko vya makusudi na wazi ili Emma aachie ngazi ila kwasababu Emma alikuwa amependa ikawa ngumu kukubali matokeo.

Pamoja Emma kipato chake kilikuwa hakitoshelezi kwa kweli alijitahidi kuingia madeni ili kutatua shida za Lucy ambae hakuwa anajali kabisa bidii ya Emma
 
Huyu mhasibu aliyetajwa kwenye voice je Polisi watauchukua ushaidi? maana yalikuwa mahaba mazito mpaka Lucy alisema alipenda style za muhasibu wakiwa kwenye 6×6
 
Lakini vyovyote vile hakustahili kuuwawa.

Bora angemuacha tu maana kumuacha mtu nako ni adhabu kubwa sana na ya kutosha tu.

Halafu kusikiliza upande mmoja na kufanya hukumu naona kama si Sawa.

Pengine naye angepewa nafasi ya kujieleza labda angeweza kueleweka na jamii.
Inaonekana jamaa hakuplan kuua, mzozo uliotokea gest ukute jamaa alimpiga na kitu demu akazima, ndio mchizi akajiongeza kusepa kwenda katavi
 
Mapenzi ya upande mmoja, na kutokuwa na kipato.

Kwa nilivyozisikiliza Lucy hakuwa na mapenzi na Emma, Emma alikuwa analazimisha mapenzi na mbaya zaidi Lucy amemfanyia Emma vituko vya makusudi na wazi ili Emma aachie ngazi ila kwasababu Emma alikuwa amependa ikawa ngumu kukubali matokeo.

Pamoja Emma kipato chake kilikuwa hakitoshelezi kwa kweli alijitahidi kuingia madeni ili kutatua shida za Lucy ambae hakuwa anajali kabisa bidii ya Emma
Lakin kuna audio moja Emma anamuuliza kama bado wanaendelea na uhusiano wao, Lucy akamwambia wapo pamoja... Bora angemchana live aumie yaishe kuliko kumkubalia halafu rohoni hamna kitu
 
Jamaa aliyejulikana kwa jina la Jerome,amemuua mke wake aliyekua anajulikana kwa jina la Lucy na kisha kujiua.Jamani kama huwezi kuachana na ex wako,usiolewe,na kama ukiolewa,achana na ex wako.
Ukisikiliza hii VN unaweza hata ukatumia njia ya maumivu katika kutekeleza haya mauaji ya uyu mwanamke.apumzike kwa amani mwamba
 
Back
Top Bottom