Pre GE2025 Rukwa: Kijiji cha Kanazi kunufaika mradi wa maji ya kisima

Pre GE2025 Rukwa: Kijiji cha Kanazi kunufaika mradi wa maji ya kisima

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Naibu waziri wa Maji, Kundo Andrew Mathew amefanya ziara ya kikazi katika halmashauri ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa katika ziara hiyo Naibu Waziri wa Maji pia ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji Mkangale na amekagua mradi wa maji mtaa wa Isunta akiridhishwa na utekelezaji wake.

Kutokana na mradi wa maji uliopo kijiji cha Kanazi kutoanza kutoa huduma ikamlazimu Naibu Waziri wa maji Kundo Mathew kutoa maelekezo ya Serikali kuwa siku tano RUWASA mkoa wa Rukwa iwe imekamilisha matengenezo madomadogo ili wananchi wanufaike na matunda ya mradi huo.

Soma pia: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Mhadisi Bruno Isakwisa, Mratibu wa Programu ya visima 900 mkoa wa Rukwa akieleza taarifa ya Mradi huo akisema visima saba (07) vinavyochimbwa katika halmashauri ya wilaya ya Nkasi l

Kwa upande wao Wakazi hao wa kijiji cha Kanazi wamempokea Naibu Waziri wa maji Mhandisi Kundo Mathew kwa nderemo na vifijo wakiwa na matumaini ya kuanza kupata huduma ya maji ambapo Wametoa kilio hicho wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa maji wa kijiji cha Kanazi.

Wakazi wa kijiji cha Kanazi wilaya akiwemo Ludis ulaya na Stela Kwimba wamemuomba Naibu Waziri wa maji Mhandisi Kundo Andrew Mathew kuharakisha upatikanaji huduma ya maji kwenye mradi wa visima 900 alioweka jiwe la msingi ili kuwapunguzia adha ya wananchi ya kutafta maji zaidi ya kilomita saba (7).
Screenshot 2025-03-04 151215.png
Screenshot 2025-03-04 151142.png
Screenshot 2025-03-04 151159.png
 
Back
Top Bottom