Lenie
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 17,229
- 50,144
Kuficha mtoto na kumfanyia vitendo vya kishirikinaNini inatia hasira? Kupigwa mawe au kuficha mtoto?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuficha mtoto na kumfanyia vitendo vya kishirikinaNini inatia hasira? Kupigwa mawe au kuficha mtoto?
Na hao wahuni ndio wanaichafua serikali ya awamu ya tano, siunajua haohai ndio walitengeneza ile sinema ya lisu halafu wakaisingizia serikali kupitia wasiojulikana?Haya ni mauaji ya kikatili sana haikubaliki Jeshi la polisi lifanye liwasake hao wahuni.
Halafu kuna wabishi eti ushirikina au uchawi haupo. Eti nini? Hayajawakuta tu.JESHI la Polisi mkoani Rukwa linawasaka watu wasiojulikana kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga mawe, mwanamke aliyefahamika kwa jina la Maria Birika (40), mkazi wa Kijiji cha Myunga, Kata ya Mkali, wilayani Kalambo.
Imeelezwa kuwa watu hao wamemfanyia kitendo hicho kwa kumtuhumu kujihusisha na vitendo vya kishirikina.
Tukio la mauaji ya mwanamke huyo lilitokea Juni 26, saa 12:00 jioni baada ya watu hao kufika nyumbani kwake na kumkuta mtoto aliyefahamika kwa jina Given Lameck (15), akiwa amefungiwa nyumbani kwa mwanamke huyo, huku akiwa amefungwa kitambaa chekundu usoni.
Kabla ya mauaji hayo, mtoto Given alipotea nyumbani kwao katika mazingira ya kutatanisha, ndipo harakati za kumtafuta zilianza, na kwamba ndugu zake walimtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masejo, alisema baada ya jitihada za kumpata mtoto huyo kushindikana, waliamua kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji kisha kuendelea kumtafuta.
Alisema baada ya kumtafuta kwa muda mrefu walifanikiwa kumkuta nyumbani kwa mwanamke huyo akiwa amefungiwa ndani na amefungwa kitambaa chekundu usoni, huku akionekana kana kwamba amechanganyikiwa kutokana na kuongea vitu visivyoeleweka.
Baada ya kupatikana kwa mtoto huyo, ndipo watu waliokuwa wakimtafuta walipo hamaki na kushikwa na hasira na kuanza kumpiga mwanamke huyo kwa mawe na vipande vya matofali vilivyokuwa karibu na nyumba yake na kumsababishia majeraha makubwa, kuvuja damu nyingi na kufariki dunia kutokana na kukosa matibabu ya haraka.
Kamanda Masejo alitoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Rukwa kuachana na imani za kishirikina katika matukio yanayotokea mkoani humo, kwa kuwa imani hizo zimekuwa chanzo cha vifo vingi vinavyotokana na kujichukulia sheria mikononi.
Chanzo: IPP Media
We unatapika tu hata visivyotapikwaHaya ni mauaji ya kikatili sana haikubaliki Jeshi la polisi lifanye liwasake hao wahuni.
Kweli mkuuHahaha inashangaza sana, jeshi letu kila siku linaua watuhumiwa, utasikia alitaka kutoroka akapigwa risasi, wakati wakifahamu sio kweli.
Wanatofauti gani na wananchi kumuua mtuhumiwa wa uchawi?!
Wewe uliishaibiwa?je ukimkamata mwizi wako utamfanyaje?utampa soda na chips ale au utampa kipondo?hebu ongea ukweli,,, mfano,,,mama yako kapotea kwenye mazingira ya utata,,,baada ya muda mwanao nae anapotea,,mnatafuta kwa muda kadhaa,,mnafanikiwa kumkuta kwa mama Fulani,,akiwa kamgeuza msukule mtoto wako,,, sasa utachukuwa hatua gani?Huwa nashangaa sana michango ya watu humu wanaojifanya eti ni werevu kumbe n wajinga wa kutupwa.
Ushirikina upo sana Rukwa hasa maeneo ya vijijini waliowahi kuishi huko wanaweza kuwa mashuhuda wazuri wa hayo mambo.
NB:kila binadamu ana haki ya kuishi sikubaliana kabisa na kitendo cha watu kujichukulia sheria mkononi
Duu,,kumbe kuna hadi andiko,,,maana yake hao wanainchi wametenda jambo jema kabisa kwa MUNGUWametimiza mahandiko
Kutoka 22:18
"Usimwache mwanamke mchawi kuishi. "
Halafu hiyo serikali ndy tatizo kubwa kabisa,,,Mimi mkuu yalinikuta matatizo kama hayo,,,halafu matokeo yake yule niliyemtuhumu uchawi akaenda police kupindua kesi nataka kumuua..duu,,police walinisumbuwa sn tu...Halafu kuna wabishi eti ushirikina au uchawi haupo. Eti nini? Hayajawakuta tu.
Kwa walioua au kwa wanaoficha watoto wa watu?Elimu itolewe ya kutosha.
Mkuu Mimi kuna jirani yangu mmoja nikimtuhumu uchawi,,matokeo yake akapinduwa kesi police nimetishia kumuua,,,,nilisumbuka sana hadi kufuta kesi...Hii si ndio ile principle ya "kulaza chini" ama?
Ukilikuta jambazi "unalilaza chini".
Kama majambazi wanaopora tuvitu tudogo dogo wanalazwa chini bila mjadala, seuze jambazi linalopora binadamu na kuwafanya misukule?
Huyo alazwe chini tu. Tumechoka ushirikina!
Siku za nyuma nilikuwa siamini kabisa uwepo wa mambo ya ulozi mpaka niliposhuhudia mwenyewe!
Wachawi wanakera sana wacha washughulikiwe tu!
Hawafai hao!Mkuu Mimi kuna jirani yangu mmoja nikimtuhumu uchawi,,matokeo yake akapinduwa kesi police nimetishia kumuua,,,,nilisumbuka sana hadi kufuta kesi...
Wakati nipo south Africa,,,kuna Dada Fulani jirani yangu alinitumia text,,akanambiya jirani namuona mama wa nyumba ya jirani yako anafukia vitu getini nyumbani kwako,,,sababu ni usiku na hanioni,,ila anafanya vitu sivielewi hapa getini,,,anachimba na kufukia vitu,, na kwa kweli wakati nipo kule nilipata mikosi sana tu ,,nilipoteza zaidi ya maelfu ya rands kimikosi mikosi tu,, basi niliporudi nilitafuta mbinu nikamwambiya yule mama,,kesho naleta mganga hapa nyumbani au utoe vitu ulivyoviweka hapa getini,,,aisee,,muda sio muda yule mama katoka mbio kaelekea police,,,kufika kapindua kesi nimetamka nataka kumuua,,duu,,kesi ilinimalizia sana pesa,,,kwahyo mkuu walozi wapo na hawaatahili kuishi,,wakaishi dunia yao huko mbele ya safari...huyo mama angebakishwa angesingizia hata wamembaka,,,na upotevu wa Mali ...
Hatari mkuu,,,matokeo yake ananipiga kimya kimya,,, wachawi watu wabaya sn,,,sio wa kuwachekea,,,pengine mkuu ulipaswa uwe hata mteule wa rais,,,lakini wachawi wamekupeleka shughuli zingine...ha ha ha ha..nuksi tupu hawa..Hawafai hao!
Viongozi wa dini hasa walokole ndiyo wanafanya watu waamini ushirikina zaidi. Mahubiri yao yote yanalenga kumfanya muumini aamini ushirikina ni tatizo kubwa sana katika nchi yetu. Matokeo yake watu wanaishia kuamiani kila kitu ni ushirikina.viongozi wa dini ktk eneo hilo mnakazi ya ziada ya kulingania neno la Mungu
Hahahaa...Hatari mkuu,,,matokeo yake ananipiga kimya kimya,,, wachawi watu wabaya sn,,,sio wa kuwachekea,,,pengine mkuu ulipaswa uwe hata mteule wa rais,,,lakini wachawi wamekupeleka shughuli zingine...ha ha ha ha..nuksi tupu hawa..
Kweli mkuu,,itolewe elimu watu waache uchawi..vinginevyo tutawapa vipondo kila siku @#$%& zao wachawi na wanga woteElimu
Elimu
Elimu