Rukwa: Nyuki waua mmoja Sumbawanga

Rukwa: Nyuki waua mmoja Sumbawanga

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
259
Mwanamke mmoja aitwaye Janath Swedi (72) Mkazi wa Mtaa wa Mtakumbuka, Kata ya Momoka Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa, ameuawa kwa kushambuliwa na kundi kubwa la nyuki nyumbani kwake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mwenyekiti wa Mtaa huo, Mohamed Makubi amesema tukio hilo lilitokea mtaani kwake Julai 10, 2023 na jitihada za kumuokoa Mwanamke huyo zilifanyika akapelekwa Hospitali lakini ilipofika majira ya saa nane usiku wa kuamkia Julai 12 alifariki.

Diwani wa Kata ya Momo, Charles Chakupewa amekiri kutokea kwa tukio hilo.

CHANZO: Millard Ayo
 
Nyuki wanatengeneza asali, kitu kitamu ila ukiwachukulia poa ni wakali hasa wanapokuwa wana asali huchachamaa kushambulia anayekaribia na kujaribu kuwachokoza wanapokuwa wametulia wakilinda masega yao ya asali. Nyuki wakikasirika hushambulia yeyote aliye karibu nao anayeonekana tishio kwao.
 
Nyuki wanamtiti,hasa wakijua unataka kuharibu maskani yao,au kumdhuru malkia wao,Tahadhari wakianza kukushambulia timua mbio,Wala usijaribu jigaragara chini,ukadhani wataacha,kimbiiiiiaa mbali na anga zao.
 
Nyuki wanamtiti,hasa wakijua unataka kuharibu maskani yao,au kumdhuru malkia wao,Tahadhari wakianza kukushambulia timua mbio,Wala usijaribu jigaragara chini,ukadhani wataacha,kimbiiiiiaa mbali na anga zao
Ukilala chini nyuki hawakuumi. Wanapitiliza.
 
Bi Janeth Sued mwenye umri wa miaka 72, mkazi wa mtaa wa Mtakumbukwa, Kata ya Momoka Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa ameuawa kwa kushambuliwa na kundi la nyuki nyumbani kwake.

Mashuhuda mmojawapo akiwa ni mtoto wa marehemu wameeleza kuwa walikuwa wameketi nje ya nyumba na Mama yake (Sasa Marehemu) ndipo nyuki mmoja alianza kuwasumbua hali iliyopelekea Mama yake kumfukuza na akatoweka.

Anaeleza kuwa baada ya muda kidogo alipita Mama mmoja akiwa amebeba miwa na baada ya muda alirudi mbio akiwa amebeba mtoto huku kundi la nyuki likimfuata kwa nyuma.

Kutokana na uharaka wa tukio anaeleza walishindwa kumtoa Marehemu kwa haraka na ndipo katika jitihada za kujiokoa akaelekea upande waliokuwepo nyuki wengi zaidi ambao walimshambulia kwa wingi

Majirani walimpeleka hospitali akapatiwa huduma na kurejea nyumbani ambapo mauti yalimfika.
 
Mwanamke mmoja aitwaye Janath Swedi (72) Mkazi wa Mtaa wa Mtakumbuka, Kata ya Momoka Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa, ameuawa kwa kushambuliwa na kundi kubwa la nyuki nyumbani kwake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mwenyekiti wa Mtaa huo, Mohamed Makubi amesema tukio hilo lilitokea mtaani kwake Julai 10, 2023 na jitihada za kumuokoa Mwanamke huyo zilifanyika akapelekwa Hospitali lakini ilipofika majira ya saa nane usiku wa kuamkia Julai 12 alifariki.

Diwani wa Kata ya Momo, Charles Chakupewa amekiri kutokea kwa tukio hilo.

CHANZO: Millard Ayo
Siku ikitokea nkashambuliwa na nyuki wawili tu najua ndo mwisho wangu wa maisha
 
Mwanamke mmoja aitwaye Janath Swedi (72) Mkazi wa Mtaa wa Mtakumbuka, Kata ya Momoka Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa, ameuawa kwa kushambuliwa na kundi kubwa la nyuki nyumbani kwake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mwenyekiti wa Mtaa huo, Mohamed Makubi amesema tukio hilo lilitokea mtaani kwake Julai 10, 2023 na jitihada za kumuokoa Mwanamke huyo zilifanyika akapelekwa Hospitali lakini ilipofika majira ya saa nane usiku wa kuamkia Julai 12 alifariki.

Diwani wa Kata ya Momo, Charles Chakupewa amekiri kutokea kwa tukio hilo.

CHANZO: Millard Ayo
Mleta mada type source of information

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom