Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
Serikali ya Tanzania kupitia TANROADS inajenga mradi wa barabara ya Ntendo- Muze-Kilyamatundu (Km 179) mkoani Rukwa kwa kiwango cha lami.
Akizungumza mara ya baada ya kutembelea mradi huo, unaojengwa na kampuni ya China Geo – Engineering
Corporation Ltd (CGC) leo Aprili 30-2023 Waziri Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema mradi huo unajengwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza ni ujenzi wa KM 25 kwa gharama ya Shilingi bilioni 45.299.
Amesema Rais wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa sana na mpaka sasa hakuna mradi wowote Nchini ambao umesimama kwa sababu Mkandarasi hajalipwa, wote wanalipwa kwa wakati na kazi kwenye miradi ya barabara na miradi mingine wanaendelea kulipwa.
"Hivi karibuni Serikali kupitia TANROADS tunakwenda kusaini miradi ya EPC plus Finance, tutasaini zaidi ya kilometa 2000 kwa wakati mmoja, haijawahi kutokea tangu Nchi hii iundwe, wastani kwa mwaka tulikuwa tunasaini miradi ya kilometa 150/160 Tanzania nzima kwa upande wa barabara, lakini sasa tunakwenda kusaini Km 2000 kuunganisha mikoa yote, tuendelee kumpa ushirikiano Rais wetu na kuhakikisha miradi hii inakwenda vizuri" amesema Waziri Mbarawa.
Akitoa taarifa fupi ya mradi Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila amesema Mradi huo unaanzia kwenye Kijiji cha Ntendo kwenye makutano ya barabara kuu ya Sumbawanga - Mpanda na barabara ya Mkoa ya Ntendo – Muze na kuishia Kijiji cha Kizungu.
Amesema barabara hiyo inapita eneo lenye fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kilimo, ufugaji,uvuvi, uchimbaji madini (makaa ya mawe) na uchimbaji wa gesi na kwamba barabara hiyo inaunganisha mikoa ya Songwe, Rukwa na Katavi kupitia bonde la Ziwa Rukwa, ambayo ni maeneo muhimu kwa shughuli za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi.
Ameongeza kuwa ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa Kilomita 25, upana wa mita 9.5, mita 1.5 kila upande ni kwa ajili ya watembea kwa miguu na mita 6.5, kwa ajili ya magari na kwamba Utekelezaji wake umefikia asilimia 23.
Aidha muda wa mradi huo ambao ujenzi wake unajumuisha pia ujenzi wa makalavati makubwa 17 na makalavati madogo 43, ni miezi 18, umeanza tarehe 6 Juni 2022 na unategemewa kukamilika Disemba mwaka 2023.