Rukwa: Waganga 170 wakamatwa, wengine walikuwa wakifanya mapenzi na wake za watu

Rukwa: Waganga 170 wakamatwa, wengine walikuwa wakifanya mapenzi na wake za watu

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwalaghai wananchi kuwa wana uwezo wa kuwatambua na kuwaadhibu wachawi, kusafisha nyota na kufufua wafu hivyo kusababisha chuki, husuda, na taharuki.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Theophista Mallya, waganga hao wanakuwa na kioo kinachodaiwa kutambua kama kuna uchawi au mchawi ndani ya nyumba.

Aliongeza kuwa “Kuna wananchi kwa hiyari yao wenyewe wanawapatia wasichana wenye umri mdogo kushiriki nao mapenzi huku wanaume wengine wakiwa radhi waganga hao kufanya tendo hilo na wake zao".

=====================

Jeshi la Polisi mkoani Rukwa limewakamata waganga wa kienyeji 170 maarufu kwa jina la lambalamba wakiwamo wanawake 37 wanaotuhumiwa kujishirikisha na ramli chonganishi

Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwalaghai wananchi kuwa wana uwezo wa kuwatambua na kuwaadhibu wachawi, kusafisha nyota na kufufua wafu hivyo kusababisha chuki, husuda, na taharuki.

Inadaiwa kuwa lambalamba ‘wamevamia’ Mkoa wa Rukwa wakitoka mikoa ya Lindi, Morogoro, Kigoma na nchi jirani ya Zambia. Huwatoza wananchi hadi Sh milioni 10 yakiwa ni malipo ya huduma ya kuondoa uchawi kwenye nyumba na kuwatambuwa wachawi na kuwaadhibu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa,Theophista Mallya alilieleza HabariLEO kuwa waliwakamata ‘lambalamba’ katika msako uliofanyika katika vijiji 17 vilivyopo katika wilaya za Kalambo na Nkasi.

Alisema lambalamba 95, wanaume wakiwa 61 na wanawake 34, walikamatwa wilayani Nkasi. Walikamatwa katika vijiji vya Kabwe, Kipili, Miovu, Nkana, Wampembe na King’ombe vilivyopo wilayani Nkasi.

Wilayani Kalambo walikamatwa 75 ambao kati yao, 72 ni wanaume na wanawake watatu waliokamatwa katika vijiji vya Zyangoma, Serengoma, Kilesha , Kasanga, Kapozwa, Mpombwe na Samazi

Kamanda Mallya alisema katika msako huo pia vifaa vilikamatwa vikidaiwa kutumiwa na watuhumiwa hao. Navyo ni vinyago,vibuyu, tunguli, dawa za miti shamba, vipaza sauti na ngozi za wanyamapori.

“Inadaiwa kuwa lambalamba anapoingia ndani ya nyumba anakuwa ameshikilia kioo ambacho kinadaiwa kuwa na ‘sensor’ (utambuzi) inayotambua kama kuna uchawi au mchawi ndani ya nyumba, ” alisema.

Aliongeza “Mbaya zaidi wananchi kwa hiyari yao wenyewe wanawapatia wasichana wenye umri mdogo kufanya nao mapenzi huku wanaume wengine wakiwa radhi lambalamba kufanya mapenzi na wake zao”

Mallya aliomba viongozi wa dini waendelee kuwaombea na kuwaelimisha waumini wao ili wawakomboe kutoka kwenye kuamini lambalamba.

Alisema wengi wa waganga hao, wanahifadhiwa katika vijiji na visiwa vilivyo katika mwambao mwa Ziwa Tanganyika katika wilaya za Nkasi na Kalambo ambavyo havifikiki kwa urahisi.

HABARI LEO
 
Daah, Ngoja na mimi nitafute tunguri niingie kazini , Yaani unamkula nke ya mtu na unalipwa ?
 
Ila waganga wanawatafuna sana wake na madem za watu [emoji1]
Wengine mpaka jicho wanaliwa

Ova
 
Katika viumbe waliokosa akili, basi wanawake wanaongoza kwa kushikiwa akili. Reasoning capacity ya wanawake wengi ni below average.

Wengi wanafanyiwa vitu vya hovyo kwa sababu za kijinga kabisa.
 
Kuna mahali hapa wanapiga kazi mpaka muda huu, mama mmoja kawaita mwenyewe nyumbani kwake ili wasafishe nyumba ila baada ya kutoa kilichoitwa msekure, mama akanyweshwa dawa na kuwa chizi hapo hapo huku wananchi wakishangilia kuwa ni mchawi na hataishi tena! [emoji2][emoji2]
 
kwa hiyo kama una wife alishaenda kwa mganga sumbawanga, jua ameshaliwa na mganga. tena watu wa kule nasikia huwa hawakati goviz.
 
Wachawi wanatesa sana watu aisee, sikieni tu hawa wachawi !

Hao lambalamba wapo tangu zamani Ila sasa hao lamba lamba wengi sikuhizi wameingiza tamaa ya pesa na anasa.
 
Nimemkumbuka yule mganga jirani mzee paulo... alikua anawalamba (anawapa tiba) kwenye gari bovu
 
Kama hawakubakwa hayo ni makubaliano. Waganga waachwe wawapeleke wajinga wenzao kuzimu
 
Kama hawakubakwa hayo ni makubaliano. Waganga waachwe wawapeleke wajinga wenzao kuzimu
huyo mjinga si ukute ni waifu wako mzee, ameenda kupata dawa ya kukushika wewe masikio. dawa ni kupiga vita uganga kabisa.
 
binafsi huwa simkubali Bashiru, wala polepole, wala sabaya, wala bashite and the likes. ila pia, huwa sikubaliani na watu wanasifu tuuu, wakati hela inayotumika sio ya mtu binafsi ni ya serikali, ni ya kweli yaani. ningekuwa mimi ndio rais, ningewaambia watu waache kusifu na kuabudu.
 
Back
Top Bottom