Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
MKUU wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Carlolius Misungwi, ametoa siku 16 kwa watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha wanarejesha Sh. milioni 162 ambazo ni makusanyo ya halmashauri hiyo ambazo wanadaiwa kuzitumia kwa matumizi yao binafsi.
Amesema wakishindwa kurejesha fedha hizo, watakamatwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Misungwi alitoa agizo hilo jana kwenye kiako cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo lililoketi kwa ajili ya kupitisha mpango na bajeti ya mwaka wa fedha wa 2021/22.
Alisema kuwa tangu halmashauri hiyo ilipoanza utaratibu wa kukusanya mapato kwa mashine za kielekroniki na kuyapeleka benki, watendaji hao wamekuwa na tabia ya kutopeleka fedha hizo benki, badala yake wamekuwa wakitumia fedha mbichi kwa matumizi yao binafsi.
Misungwi alisema katika halmashauri hiyo, watendaji 93 wametumia Sh. 162,742,350 (milioni 162.7), hivyo kuwataka wazirudishe kabla ya Februari 28, vinginevyo ataliagiza Jeshi la Polisi kumkamata kila mtendaji anayedaiwa.
"Ninaagiza kuanzia leo (jana) hadi Februari 28, kila mmoja arudishe kiasi cha fedha anazodaiwa, ikipita tarehe hiyo nitampa orodha OCD inayoonyesha kila mtendaji kiasi anachodaiwa na kijiji alichopo na nitamwagiza amkamate ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake," alionya.
Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, Daud Sichone, alisema baraza linaunga mkono agizo la Mkuu wa Wilaya huyo kwa kuwa halipo tayari kuona watendaji wa serikali wanaongoza kuhujumu kodi za wananchi.
Alisema kuwa tangu mwaka 2017, fedha ambazo hazijapelekwa benki kutokana na makusanyo hayo ni Sh. milioni 300 na kwamba baadhi ya wadaiwa wameshastaafu, wengine wamefariki dunia na wengine kufukuzwa kazi kwa makosa mbalimbali.