Rundo la vidonge vimetupwa mtaani, naenda kuwaeleza serikali ya mtaa

Rundo la vidonge vimetupwa mtaani, naenda kuwaeleza serikali ya mtaa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Nataka nipime uwajibikaji wa serikali. toka asubuhi nimeona kuna rundo la madawa yametupwa barabarani kabisa Jambo ambalo ni hatari madawa yenyewe yanafanana na Yale ya minyoo watoto wakiyaona watadhani ni pipi sijui ndo yame expire au vipi.

Me siwezi kujitolea kuanza kuyaokota sio kazi yangu hiyo ni kazi ya manispaa. Karibia gunia zima la vidonge.

Ngoja ni-attach picha yake.

2902046_IMG_20210828_124948.jpg
 
Una uhakika sio hizi chanjo mpya za vidonge zimeingia?
 
Viko vingi Sana kwenye likiroba. Nimeenda ofisini mwenyekiti hayupo kaenda sijui kanisani. Sasa Mimi bado sijafikia uzalendo wa kiasi Cha kuzoa

IMG_20210828_124948.jpg
 
Mkuu Mbona unajisumbua. Wewe jali maisha yako na familia yako.
Acha wazile tu hazina athari kwa mmatumbi kwasababu immunity ya mmatumbini bishi na imezoea shida na misukosuko. Mbona sisi tangu udogoni tunakula hayo mavitu na bado tunadunda tu
 
Alafu unataka kuwa dadali kwa ubea huu? Wee kazi huwezi mpaka hapo usashindwa
 
Hahaha mkuu kaburi halina hata siku ushalifukua duh acha uchawi ule Ni Uzi mwingine na huu Ni Uzi mwingine
Pamoja na hayo unajua kabla hujamkabidhi askari silaha unamtreing kwanza hadi aive sasa wewe hata hujala kiapo ushaanza kutoa siri
 
Mkuu kuwa na utu kidogo.utani usiwe uzidi kihivyo
Huwezi kuwa na utu kwenye jamii haijijali na kukujali. Akienda kuripoti ataambiwa anajipendekeza na hawstafuatilia. Ni Mungu tu ndo utusaidiaga. Wacha tu madogo wazile tu.
 
Nataka nipime uwajibikaji wa serikali.toka asubuhi nimeona kuna rundo la madawa yametupwa barabarani kabisa Jambo ambalo Ni hatari madawa yenyewe yanafanana na Yale ya minyoo watoto wakiyaona watadhani Ni pipi sijui ndo yame expire au vipi.me siwezi kujitolea kuanza kuyaokota sio kazi yangu hiyo ni kazi ya manispaa..karibia gunia zima la vidonge.ngoja Ni attach picha yake.
Toa taarifa kwa Afisa Afya wa eneo lako au Afisa Mtendaji.
 
Hiyo ni roho mbaya. Siku utapata matatizo hapo kwako majirani wakuache upambane mwenyewe. Punguza ubinafsi wewe, jali wengine na wewe utajaliwa in return!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata hao majirani kukusaidia ukipata matatizo siyo kupenda kwao ni msukumo wa Mungu. Mtanzania kukusaidia siyo kwa hiari ni msukumo wa kimbingu (divine intervention).
 
Back
Top Bottom