Rungu la TCRA lawashukia Wasafi Tv, Clouds FM, Carry Mastory, Radio one na RFA kwa kurusha maudhui yaliyo kinyume na Sheria

Rungu la TCRA lawashukia Wasafi Tv, Clouds FM, Carry Mastory, Radio one na RFA kwa kurusha maudhui yaliyo kinyume na Sheria

Ila hawa jamaa wamezidi matusi utadhani vijana wanaobarehe ndo wajitafakari kipindi kinauzia jina ila hakuna chochote
 
What a stupid redio programe? Unazungumzia mambo ya kujichua kwenye kipindi ambacho hata watoto wanasikiliza? Jamaa wa jahazi walijisahau sana.
 
Kwa sasa ni vipindi vya kusifu a.k.a. mijisifa tu, binadamu anasifiwa kuliko hata Mwenyezi Mungu muumba wa vyote!
 
vyombo vya habari vinatulazimisha kwa nguvu tuwe kama Westerners, wanadhani ndio fashion ya dunia ya leo
 
TCRA imetoa onyo kali na kuziweka chini ya uangalizi wa miezi mitatu Radio Free Africa na Radio One Stereo kwa kukiuka kanuni za utangazaji viliporusha kipindi cha Amka na BBC ambapo Tundu Lissu aliituhumu serikali kuwazuia viongozi wa Chadema kumuaga Hayati Rais Benjamin Mkapa.

Wasafi Media Online TV imetuhumiwa kurusha maudhui yanayochochea vitendo vya ngono kupitia kipindi cha Women Matters. Kosa la ngono kamati imetoa onyo na faini ya milioni 5 itakayolipwa TCRA.

Kamati ya Maudhui ya TCRA imekifungia kipindi cha Jahazi Cha Clouds FM kwa kosa la kurusha maudhui yenye kuchochea kujichua sehemu za siri na ngono. Aidha, Clouds FM imetakiwa kutokujaza muda huo kwa kipindi kingine chenye maudhui sawa na Jahazi

Chanzo:
TBC Online
Speechless.
 
Gadner G habashi Hana tafsida wala break kutaja maneno. Kama Jana alitamka neno SHAHAWA, Mara nyingi Sana maneno ya ngono huwa anatamka bila wasiwasi Kama chupi,mavi,shahawa,demu,kujichua,malaya,tendo LA ndoa linavyofanyika etc ambayo hayana staha.. Mimi naona jahazi na clouds hawajaonewa kabisa
 
Hapo kwa jahazi ni sahihi kabisa hajaonewa mtu, nilitegemea hili panga na limefika haswaaa.

Kati ya kipindi ovyo kabisa kuwahi kuwepo ni jahazi tena kuwepo yule jamaa sijui ndiye anaitwa gadina, yeye aliona matusi/kejeri ndiyo master of program.
 
Vizuri sana, wapige marufuku hata singeli zinazocheza hovyo, tunataka jamii yenye maadili, tcra kwa mara ya kwanza ninawapongeza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuanzia asubuhi waw wanawahoji wakina gigy money, shilole juma lokole Kumbuka tu ndy mambo watu wanatakiwa kusikia sahv

Ova
 
Daaah clouz kusema kwelii waamke kwenye usingizi wasipoo angalia hii redio inakujakua kama tbc taifa walahi

Janja zao za kuwa laghai vijana na vipindi pind vyao na kushobokea chama tawala watu wamezigundua wanafikiri bado wanaishi kwenye zama za JK.

Magu alisema mwenye hii nchi inaongozwa kisheria naoan kunabathii wa "nyumbu" hawajamwelewe vizuri. naanukuu bathi ya maneno yake "hata Mke wangu akifanya kosa awekwe ndani"

Sasa kama ameshasema mkewe tu awekwendani sembuse clous ambayo hana hata ndugu hapo.

Hiv ndo vitu namkubali sana Rais magu kwa kusimamia japo anampapungufu yake.
 
Back
Top Bottom