RUNGU: TCRA imeitaka Wasafi TV kusitisha matangazo kwa Miezi Sita (6) kuanzia leo kwa kurusha Maudhui ya utupu

RUNGU: TCRA imeitaka Wasafi TV kusitisha matangazo kwa Miezi Sita (6) kuanzia leo kwa kurusha Maudhui ya utupu

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
TCRA imeitaka Wasafi TV kusitisha kurusha matangazo kwa miezi sita kuanzia leo kutokana kwa kukiuka kanuni za utangazaji kwa kurusha maudhui ya utupu.

Maamuzi hayo yanakuja kufuatia maudhui ya picha jongefu yaliyomwonesha msanii wa bongo Fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money akicheza ‘utupu’ kinyume na Kanuni katika tamasha la “Tumewasha Live Concert” lililorushwa Januari Mosi 2021 kuanzia saa mbili hadi saa tano usiku.

Aidha Wasafi Tv wanatakiwa kutumia siku ya leo kuomba radhi kwa watazamaji wake kufuatia ukiukaji huo na wakikaidi hatua zaidi za kisheria na udhibiti zitachukuliwa.

Pia soma >
Gigy Money kafanya nini huko kwenye ziara ya Tumewasha na Tigo?
 
Giggy Money Giggy Money...nakuita Giggy Money!

Wasafi wajinga SANA au vile walikuwa kwenye kampeni za mi5 tena, wakafikiri wanaweza fanya chochote?? Walishakuwa washikaji na watawala?

Haya tuwatakie kila la heri!
Kila mtu anaisoma namba! Wengine za kigiriki na kiebrania tushazimasta!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Hao TCRA itabidi wapunguziwe mamlaka, itakuwa wanatumika tu na washindani wa kibiashara wa watu.

Miezi sita as if wametangaza kupindua serikali.

Hizo ni ajira za watu na ni uwekezaji pia lazima adhabu zizingatie na hayo.
 
Back
Top Bottom