Rungwe: Moja ya Wilaya zilizosahaulika na masikini zaidi Tanzania

Mtoa mada nakubaliana na wewe kwenye suala la umaskini wa kimaendeleo , suala la wananchi wa Rungwe kuwa mbali na elimu napinga. Mimi ni kijana mzaliwa wa Rungwe na nimekulia huko, na primary mpaka secondary nimesoma huko, maendeleo yapo nyuma Sana tena ile Sana.
Wananchi wanaishia kupewa ahadi za uongo kipindi Cha uchaguzi na hakuna mabadiliko yoyote kipindi Cha uongozi wao. Na mwisho vijana wengi wa Rungwe wamesoma lakini elimu yao/yetu bado haijasaidia kitu kwenye kuinfluence maendeleo. #ndaghafijho
 

Msijitetee. Rungwe haikupaswa kuwa na hali iliyonayo sasa hivi ya kujisifia mambo ya kihistoria. Rungwe inatakiwa kulinganishwa na Kilimanjaro sio Kongwa. Pokeeni criticism muifanyie kazi.

Amandla....
 
Rungwe inahitaji mbunge wa upinzani mbunifu wa kuwasemea bungeni maana wote waliopita na aloyepo ni mabubu hasa huyu Sauli yeye yuko bize na biashara na rushwa ndio inampitisha kwa sababu ya njaa......

Kwa taarifa tu mbunge aliyepo alikua ameshindwa km ilivyokua kwa mwakyembe lkn figisu za ccm zikawaokoa....... Yaani wanarungwe na wanakyela wanvekomaa km walivofanya vwawa, mbeya mjini Tunduma na momba hayo majimbo mawili yangekua chadema.

Hata sasa ccm haitakiwi kabisa rungwe
 
Naloli nkamu ..nakubali kabisa mkuu 👊
 
Huu ummbeya unakusaidia nini....unajua wilaya maskini wew au unalinganisha na wilaya ipi ya kwenu.Upo too emotional utafikiri mwanamke uliyeachika.Unaweza kua na hoja but hauko objective
 
Kweli mimi ni mjinga sawa nimekuwa victim kama wananchi wa Rungwe. Someni shule
Angalia upumbafu wako wa kukurupuka.sijui umetumia methodology gan na huo utafiti wako wa kijuha.Nina miaka 35 nimezaliwa nimekuta umem karb vijj vingi vya rungwe
 
Angalia upumbafu wako wa kukurupuka.sijui umetumia methodology gan na huo utafiti wako wa kijuha.Nina miaka 35 nimezaliwa nimekuta umem karb vijj vingi vya rungwe

Na katika hiyo miaka 35 huo umeme umewasaidia vipi kimaendeleo watu wa Rungwe ? Ndio swali linaloulizwa. Umeme mnao, maji mnayo, chakula mnacho lakini mpaka leo hamna viwanda vya kuongeza thamani ya mazao yenu!

Amandla....
 
Hivi tukuyu iko wapi mleta mada?

Rungwe hii ninayoifahamu au kuna Rungwe nyingine.

Karibu Uvinza tutee kidogo
 
Rungwe sio wilaya masikini kutokana jiogrofia yake na elimu iko vizuri.Ila nakubalina na wewe hakuna miradi ya kiserikali iliyofanyika kama wilaya mpya zingine.Wilaya hii ilitoa mchango mkubwa baada ya Uhuru kwa kilimo cha kahawa na hata sasa imezalisha nguzo nyingi zinazotumika nchi nzima lakini zinapita kwenye barabara za vumbi tangu Uhuru .Baadhi ya wapigania Uhuru kupitia Tanu asili yao ni Rungwe kama mzee Mwakangale,RIP mzee Athumani Mwangulilo RIP.Serikali itupie jicho wilaya hiyo kama zingine
 
Na katika hiyo miaka 35 huo umeme umewasaidia vipi kimaendeleo watu wa Rungwe ? Ndio swali linaloulizwa. Umeme mnao, maji mnayo, chakula mnacho lakini mpaka leo hamna viwanda vya kuongeza thamani ya mazao yenu!

Amandla....
Inawezekana hujui hata dhana ya maendeleo mpuuzi wew....eti viwanda viwanda kipimo cha maendeleo.Hyo katumba tea company,kuna kiwanda cha gas hujaona wew mbweha.
 
Nakubaliana na ww kuhusu kubadilisha mbunge na kubadilisha chama...wana rungwe twendw na Sophia Mwakagenda
 
Inawezekana hujui hata dhana ya maendeleo mpuuzi wew....eti viwanda viwanda kipimo cha maendeleo.Hyo katumba tea company,kuna kiwanda cha gas hujaona wew mbweha.
Sidhani kama wewe ni mtu wa Rungwe kweli kwa sababu watu wa kule wana heshimu wenzao. Unasifia Katumba Tea Factory ya mwaka 49! Kiwanda kingine cha Wakulima Tea Company kilichopo Mwakaleli kimefungwa kutokana na watu huko kutozalisha chai ya kutosha. Katumba, hicho cha kihistoria, kiko ICU kwa sababu ingawa kina uwezo wa ku process tani 150 za majani ya chai kina process tani 28. Na chenyewe watakifunga hivi karibuni. Watakuacha wewe na umaskini wako na matusi.

Amandla...
 
Huyu mtu aliyeleta mada hii haijui Rungwe kabisaa, haifahamu Rungwe. Eti Rungwe hakuna umeme, aaah jamani, huyu mtu mzandiki sana huyu kajembe sijui kijembe. Hata kama anataka kufanya fitina basi amekosea 'angle' ya kufanyia hiyo fitina. Bure kabisa
 
Umesema kweli lkn kwenye hayo makabila kuchangamikia elimu mapema sio kweli, ukweli ni kuwa shule ziliwafikia mapema, Wamisionari walifika mapema huko na kutapenda hivyo wakajenga shule na wenyeji wakafaidika.

Vv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…