Rungwe: Moja ya Wilaya zilizosahaulika na masikini zaidi Tanzania

Mkuu kajembe kama unasema Rungwe ni masikini sana, inawezekana umeshuka moja kwa mja toka LA. Kama sivyo, basi huifahamu Rungwe.
 
Mtoa mada umefika Rungwe ukitokea wapi? na umepitia ruti gani kufika Rungwe?. ina maana kote huko ulikopita wameizidi Rungwe?. ukifikia hatua ya kuanzisha mada kuwa Rungwe ni masikini basi wewe huijui vizuri nchi yetu.

Isije kuwa tunakulaumu bure wakati mwenzetu umetoka New York
 
Rungwe unaenda mpaka vijijin unakuta makazi safi ambayo hata wewe huna uwezo wakuja kuwa nayo.
Rungwe ipi au kuna rungwe ingine ni rungwe hii inayotoa mafuso zaidi ya 50 ya ndizi kwa siku.
Hii rungwe inayozalisha maziwa kuliko eneo lolote tz
Rungwe hii wakulima wa viazi na mbao au.
Acheni wivu rungwe ineza ikawa ndio wilaya tajiri na moja ya wilaya yenye wasomi wengi na ilikua na shule za private kipindi .
Kuna shule za misheni mingi na wazazi kipindi
 
Rungwe walichokosa ni barabara tu za rami kwenda vijijin tuseme ya kwenda mwakaleli toka katumba au mjini kwenda masokoo au mjini kwenda ruangwa ila rungwe kwangu ni wilaya bora kabisa Tanzania hii
 
Mtoa mada kwa Rungwe umezingua, huijui Rungwe wewe, kama una maslahi binafsi na utaseme kwanza kabla ya kuanika uzi wako!Hivi katika nchi hii unaifananisha Rungwe na wilaya gani katika poverty ranking?
 
Umepigwa chini kura za watia nia unataka kumchongea mbunge wao kwa akina slowslow tulia wewe. Kuna sehemu tajiri kama Rungwe angalia mabasi yao Rungwe Express.
 
Kuonyesha rungwe ni wilaya iliyo na maendeleo unapoanzia huku juu toka mbeya kila mahali unakuta miji midogo kwanzia isyonje namba one ndaga ntokela kiwira kk katumba tukuyu ushirika yote ni miji yenye hadhi ya miji ya wilaya kadhaa apa tz. Na inamakazi ya juu sana kulingana na vipato vya wananchi hasa kilimo. Rungwe haina msimu mwaka mzima Kuna pesa. Mtoa mada umechemka
 
kuhusu miundombinu nakubalianawe 100%. Kuhusu elimu umeongea upumbavu. Kuhusu umaskini pia sikubaliani nawewe
 
waende wakajifunze maendeleo Njombe kwa wenzao wanafanana hali ya hewa.
 
Ndugu kagoshima, hata kwenye miundombinu huwezi kuisema Rungwe, labda utoe mifano halisi ya District Councils zinazoizidi Rungwe
 
Cjui Ila rungwe cyo masikni kihvyo ova Niko Arusha Ila nimepigiwa kaz San pande hzo
 
unatakiwa ujilinganishe na watu/sehemu mnaoendana nao kijografia,yani leo hii Tanzania ajilinganishe na USA si utakuwa upumbavu.sasa kuilinganisha rungwe na Lindi,Kongwa na Buhigwe ambao hamuendani nao kimazingira nani anaonakana mjinga hapo?? wewe unatakiwa ujilinganishe na Moshi,Njombe na Mafinga
 
Nawewe ni mpumbavu kama wapumbavu wengine yaaani rungwe ijiringainishe na njombe badala ya kyela. Ileje. Mbeya vijijini na makete?
 
Kwa hiyo njombe moshi na mafinga zimeizidi rungwe nini
 
Kwa utafiti wa chini Rungwe ni kubwa sana maana ina halmashauri mbili wilaya moja Halmashauri kuu na Halmashauri ndogo huko Mwakaleli.Nilienda Ileje asee watu wanashangaa gari Tz hii😓
 
Mimi nadhani aliyeleta hii mada kuwa Rungwe ni maskini ni Mchagga ambaye hajatembelea wilaya nyingi Tanzania.
Ukiondoa miji mikubwa, wilaya na hasa vijiji vingi katika rural areas kweli kweli ni maskini sana. Nenda Madaba kule Ruvuma. Ardhi safi na tele hapafikiki, nenda katika wilaya nyingi za Manyara, Dodoma, Rukwa, Kigoma, Singida utaona maajabu hata viongozi waliotakiwavwatetee vijiji katika wilaya hizo hawafiki huko. Wanakuambia ah mradi usipeleke huko hufanikiwi!
Mwenzangu TANZANIA ni tajiri lakini watu wengi sana ni maskini SANA Tanzania a yetu hii. Ndiyo maana watu wanabisha kuwa Rungwe siyo maskini kwani hawa wanaobisha ni wazi wamewahi kutenbelea sehemu nyingi za Tz na wanafahamu Hali ilivyo
 
Mimi wachagga nawalinganisha kama South Africans na jinsi wanavyoiona Africa na waafrica wengine.Kama mchagga hajatembea sana akifika wilaya moja nje ya kwao anashangaa na kuona kuwa kuna umaskini mwingi. Kwa kuwa tu analingansha na Kwao!! Mama ila yetu mengi hata yake yenye utajiri wa mali nyumba hawajui kama ni kitu muhimu. Lakini mchagga labda awe maskini sana na hana mtoto mwenye uwezo ndipo atashindwa kujenga
 
Nimefika Tukuyu hadi Matema;
Nipazuri sana,natamani nimgehamia huko.
Pia hiyo barabara ya kwenda Malawi ina changia biashara nyingi maeneo hayo.
Huwezi linganisha Rungwe na maeneo mengi Tanzania.Rungwe ipo juu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…